Akizungumza
leo na waandishi habari ,Makonda amesema kuwa Mkoa wa Dar es Salaam ni
kioo kwa nchi hivyo jitihada zinaendelea ya kutafuta na kazi hiyo
itafanywa sekta kwa sekta.
Amesema
kuwa Wakuu wa Wilaya katika jiji la Dar es Salaam hakuna kufanya kazi
yeyote mpaka wamelize kutafuta watumishi hewa kwa kutumia malipo ya
watumishi kutoka taasisi za fedha (Pay Row).
Makonda
amesema idadi ya watumishi hewa 71 aliowasilisha kwa Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais –Tamisemi, Georgre Simbachawene ni ndogo katika jiji la
Dar es Salaam hivyo kazi lazima iwe endelevu.
Amesema
kuwa watumishi Hewa hawawezi wakawa wanalipwa mshahara huku wanaofanya
kazi kwa moyo mmoja wanajisikia vibaya hivyo ni lazima watafutwe na
wachukuliwe hatua na vyombo vya dola.
0 comments:
Post a Comment