Beki wa kati wa Barcelona, Gerrard Pique ameeleza sababu ya yeye kuvaa jezi iliyo na namba tatu.

Pique alisema kuwa Barcelona utaratibu wa kuvaa jezi kwa timu ya vijana na namba hiyo alikuwa akiitumia sababu alikuwa akicheza kama beki wa kati.

“Tulicheza mabeki watatu, beki wa kulia anavaa jezi namba mbili, beki wa kushoto anavaa jezi namba tano na beki wa kati anavaa jezi namba tatu,” alisema Pique katika moja ya video zake za hivi karibuni.