mourinho
Kocha wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho ameeleza azma yake ya kurejea kufundisha soka msimu ujao huku akieleza kuwa ataangalia wapi ni sehemu sahihi kwake kufundisha.

“Nataka kufanya kazi, nitafanya kazi msimu ujao, nitafikiri na kuangalia sehemu ambayo ninaitaka, ninataka kuwa sehemu ambayo naamini wananihitaji,

“Kuhitajika sehemu ndiyo jambo ninalotaka na nitaonyesha uwezo wangu baabda ya miezi michache kuongeza nguvu mpya, nitarudi na kila kitu na mengine Zaidi. Nitakwenda sehemu ambayo ninahitajika na nitajihisi kuwa huru na nitafanya kila jambo ninaloweza,” alisema Mourinho.