SERIKALI imesema kwa sasa hakuna mtu yoyote ambaye ataenda kutibiwa nje ya nchi kutokana na magojwa ya figo na moyo.
Kauli
hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa
alipokuwa fanya ziara ya maendeleo katika hospitali ya kisasa ya
Benjamini Mkapa ambayo inahusika na matibabu ya magonjwa ya figo iliyopo
katika chuo kikuu cha Dodoma mjini.
Majaliwa
alisema sababu za kutokuwepo kwa wagonjwa kutibiwa nje ya nchi ni
kutokana na kuwa na hospitali za kisasa ambazo zipo nchini.
Mbali
na kuwepo kwa hospitali za kisasa sambamba na vifaa vya kisasa alisema
wapo madaktari bingwa na wazuri ambao kwa sasa wanazalishwa hapa nchini.
Katika
ziara hiyo akizungumza na waandishi wa habari pamoja na watumishi
alisema kwamba kwa sasa si matibabu ya figo pekee bali hasha figo
kutafanyikia hapa nchini badala ya kwenda nje.
“Kwa
sasa hakuna mtu ambaye ataenda kutibiwa nje ya nchi kwa ugonjwa wa figo
wala moyo, wagonjwa wote watatibiwa hapa ndani na si kutibiwa tu bali
hata kubadilisha figo itafanyika hapa nchini.
“Serikali
kwa sasa imeweza kuimalisha huduma hiyo kwa kuweka mashine na vifaa vya
kisasa katika hospitali ya Rufaa ya Muhimbili pamoja na hospitali ya
Benjamini Mkapa iliyopo hapa (UDOM)”.alisema Majaliwa.
Alisema
kutokana na kuimalisha uwezo mkubwa wa matibabu alisema kwa sasa
wagonjwa kutoka nchi nchi jirani kama vile,
Malawi,Msumbiji,Komoro,Waganda na Wakenya wanatibiwa nchini hapa.
Mbali na hilo Majaliwa ameagiza hospitali nchini kuacha kuhamisha vifaa vya hospitali za umma kwenda katika hospitali binafsi.
Alisema
kwa sasa Hospitali ya Benjamini Mkapa ina vifaa vingi vya kisasa vyenye
uwezo mkubwa ambavyo kwa sasa vinafanya kazi ya kutoa huduma ya
matibabu ya ikiwemo ya figo, moyo na kansa.
Alisema
kuna kila sababu ya kupunguza wimbi la kutoa vifaa vya serikali
kupeleka katika hospitali binafsi.
Sifikirii kwa malengo mliyonayo hapa
mtatoa vifaa na kupeleka katika hispitali binafsi.
Aidha,
Majaliwa alisema kutokana na uwezo na ukubwa wa vifaa katika hospitali
hiyo imebidi kuvifanyia marekebisho vyumba kwa kuviimarisha ili
kuwezesha vifaa hivyo kuingia kwenye vyumba husika.
Akitoa
ufafanuzi zaidi Mjaliwa alisema kwa sasa mkandarasi anayefanya
ukarabati na kujenga vyumba vya kuwekea vifaa vya tiba anatakiwa
kuongezewa fedha na maandiko yameaandaliwa kwa ajili ya kupelekwa
bungeni ili kupata fedha.
Kutokana na baadhi ya vifaa kuhifadhiwa nje ya vyumba, Majaliwa aliwataka viongozi wa hospitali hiyo kuvilinda vifaa hivyo.
Kwa
upande wake Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na
Wazee, Dk Khamisi Kigwangalla, alisema Wizara yake inataka kufuta bajeti
kwa ajili ya matibabu ya nje ya nchi na badala yake fedha hizo
zitaelekezwa katika vituo husika vya kutolea huduma za matibabu.
Aidha badala yake kazi hiyo ya kuwapeleka wagonjwa nje ya nchi itafanywa na hospitali za kisasa zilizopo nchini.
Hata hivyo serikali kupitia Wizara yake itaondoa kabisa jukumu la kuwapeleka
wagonjwa nje ya nchi na badala yake kazi hiyo itafanywa na hospitali za
ndani.
Pia hospitali za kisasa ambazo zipo ndani ya nchi ndizo zitakazo toa kubali
cha kupeleka wagonjwa nje ya nchi pale tu watakapoona kuwa wao
wameshindwa kutoa huduma ya tiba kwa mgonjwa husika.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dk Khamisi
Kigwangalla akisalimiana na uongozi wa Hospitali ya Kisasa ya Benjamini
Mkapa iliyopo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakati wa tukio hilo..
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akisalimiana na Madaktari wa Hospitali ya Kisasa ya Mkapa wakati akiwasili kukagua Hospitali hiyo.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dk Khamisi
Kigwangalla akijadiliana jambo na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati wa
ukaguzi wa Hospitali ya kisasa ya Mkapa iliyopo UDOM.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akikagua mashine ya MRI ambayo inaendelea kufungwa
katika jengo la Hospitali ya Kisasa ya Mkapa iliyopo UDOM.
Mashine hiyo ya MRI ambayo inaendelea kufungwa katika jengo hilo la Hospitali ya Kisasa ya Mkapa.Kaimu
Mkuu wa Hospitali hiyo Profesa Gesai akimuonyesha Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa namna ya uimala wa jengo hilo pindi watakapofunga vifaa vya
kisasa vya kutibu magonjwa mbalimbali.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia chumba cha CT-SCANA ambacho kinatarajiwa kukamilika hapo baadae
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dk Khamisi
Kigwangalla akifafanua jambo kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa juu ya
Wizara ya Afya ilivyojipanga kuiendesha Hospitali hiyo ya kisasa ya
Mkapa ambayo inamiliki na Wizara kwa asilimia mia moja.
Waziri
Mkuu Kasim Majaliwa akitoa maagizo kwa Naibu Waziri wa Afya namna ya
kuindesha Hospitali hiyo pamoja na masuala mbalimbali ya kitaalam
Mkurugenzi
wa Tiba wa Wizara ya Afya, Dk. Magreth Mhando akitoa maelezo kwa Waziri
Mkuu Kasim Majaliwa katika tukio hilo la ukaguzi wa jengo hilo la
kisasa la Hospitali ya Mkapa.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dk Khamisi
Kigwangalla akito maelezo ya kitaalam kwa Waziri Mkuu Kasim Majaliwa
walipotembelea chumba cha vipimo
Waziri
Mkuu Kasim Majaliwa akitoa maagizo kwa Naibu Waziri wa Afya Dk.
Kigwangalla na watendaji wa Hospitali hiyo ya Mkapa wakati wa kuondoka
baada ya kumaliza shughuli ya ukaguzi na kuangalia maendeleo ya ke.
(Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog-DODOMA).
0 comments:
Post a Comment