Wawakilishi wa tanzania katika michuano ya kimataifa Young Africans
pamoja na Azam FC wametakiwa kujituma na kujitolea kwa asilimia 100
katika michezo yao ya mwishoni mwa juma.
Kocha mkuu wa Ndanda FC ya Mtwara Meja mstaafu Abdul Mingange
amevitaka vilabu hivyo kupambana kutokana na wapinzani wa vilabu hivyo
kuwa na uzoefu mkubwa kwenye mashindano hayo.
“Timu zote mbili zinacheza dhidi ya timu ngumu kwasababu hizo timu
zinajua faida za mashindano haya kuanzaia wachezaji, viongozi wote
wanajua faida ya mashindano hayo hilo la kwanza. Jambo la pili ni kwamba
hizi timu hazijajengeka kwa muda mfupi zimejengwa kwa muda mrefu.
Nataka nizungumzie Yanga, Pluijm ndiyo ameanza kujenga timu ambaye
anataka timu iwe ya kimataifa zaidi lakini hajafikia hapo kwasababu bado
kuna mapungufu mengi kwenye timu”.
“Al Ahly ni timu ambayo imelelewa kucheza mashindano makubwa hasa
ukiangalia historia yao wameshachukua mara 8 kombe la Afrika wakati
Yanga hawajawahi kufika hata nusu fainali. Kwahiyo si mchezo rahisi kama
watu wanavyofikiria, kuwatoa waarabu kwenye mechin mbili siyo kitu
rahisi Yanga wanakazi ya kufanya”.
“Mechi zao walizocheza kwenye michuano ya kimataifa bado hawajacheza
vizuri, watu wanaangalia matokeo hawaangalii timu inavyocheza. Nikiipima
na mechi ya Al Ahly naona shughuli ipo”.
“Azam tok alivyo rudi Stewart Hall ilinivutia ilivyocheza Kagame
lakini kile kiwango kinazidi kupotea sasa inawezekana wachezaji
wametumika sana au mwalimu inabidi abadilishe mtazamo wake kwenye timu
kwasababu hata mechi wanazocheza kwenye ligi hawajacheza vizuri bado.
Ukiangalia mechi ya mwisho dhidi ya Bidvest Wits kama wasingecheza
kwenye jua kali Azam wangepoteza mchezo ule lakini wapinzani wao
walizidiwa sana na hali ya hewa”.
“Lakini jambo la mwisho wachezaji wanatakiwa kujitoa, moja ya tatizo
ninaloliona kwa wachezaji wetu wa Tanzania ni kutojitolea kwa asilia mia
100 wenzetu wanajitolea kwa asilimia zote. Kwahiyo kama wachezaji wetu
watajitolea ninauhakika timu hizi wanaweza kuzitoa”.
“Mpira unasema 50% ni spirit, unaweza kuishinda timu ambayo ina
tactical, technical na physical approach nzuri ndiyo maana unakuta Yanga
bado inafungwa na Coastal Union”.
Yanga wanaocheza michuano ya klabu bingwa Afrika watacheza Jumamosi
dhidi ya Al Ahly kwenye uwanja wa taifa huku Azam FC wanaocheza kombe la
shirikisho wakikipiga dhidi ya Esperance kwenye uwanja wa Azam Complex,
Chamazi.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment