Kichuya alionyesha kiwango cha juu katika mwezi huo uliokuwa na raundi nne, hivyo kuisaidia timu yake kushinda mechi mbili kati ya tatu ilizocheza.
Katika mechi hizo ambazo zote Kichuya alicheza, alifanikiwa kufunga mabao mawili kati ya matano yaliyofungwa na timu yake. Alifunga dhidi ya Coastal Union kwa ushindi wa mabao 3-0, na JKT Ruvu Stars ambapo Mtibwa Sugar ilishinda mabao 2-1.
Uwezo aliouonyesha kwa mwezi huo ulisababisha Kocha wa Taifa Stars, Charles Mkwasa amwite kwa mara ya kwanza kwenye kikosi chake kwa ajili ya mechi dhidi ya Chad iliyofanyika Machi 23, 2016 jijini N’Djamena.
Washindani wa karibu wa Kichuya walikuwa washambuliaji Mbaraka Yusuf wa Kagera Sugar, na Abdulrahman Mussa wa JKT Ruvu Stars ambao pia waling’ara kwa upande wa timu zao kwa mwezi huo.
Kichuya ambaye huu ni msimu wake wa pili kwenye Ligi Kuu, kwa kunyakua tuzo ya mchezaji bora kwa Machi atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni moja) na wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom.
Wachezaji bora wa miezi mitatu iliyopita ni kiungo Thaban Kamusoko wa Yanga (Desemba 2015), beki Shomari Kapombe wa Azam (Januari 2016) na mshambuliaji Mohamed Mkopi wa Tanzania Prisons (Februari 2016).
0 comments:
Post a Comment