NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

LIVE KUTOKA TAIFA: YANGA 1-1 AL AHLY (FULL TIME)




MPIRA UMEKWISHAAAAAAA....Evouma anajirusha na kuanguka ndani ya eneo la hatari lakini wamuzi kutoka Ivory Coast anamuambia amka twende Katika dakika 2 za nyongeza, Yanga wanagongeana vizuri lakini umaliziaji unakuwa ni uleule DAKIKA 4+ ZA NYONGEZA Dk 87 hadi 89 timu zaidi zinagongeana pasi ambazo hazina manufaa kwani hakuna hata moja iliyopiga shuti lililolenga lango Dk 86, inaonekana Ahly wameridhika na walichokitaka, lakini wanalazimika kuwa makini kwa kuwa Ahly wanaweza "kuwaotea" na kuwamaliza SUB 85 upande wa Ahly, wanafanya mabadiliko ya mwisho Zacharia anatoka na nafasi yake inachukuliwa na rais wa Gabon, Malick Evouma

Dk 84, kipa Dida anamzoa beki wake Yondani wakati akiokoa mpira, lakini beki huyo anainua Dk 82, Ngoma anageuka katikati ya mabeki watatu wa Ahly, lakini shuti lake linakwenda nje SUB Dk 81, Deogratius Munish 'Dida' anaingia kuchukua nafasi ya Barthez ambaye baada ya kutibiwa amechukuliwa na kuingizwa kwenye gari la wagonjwa
Dk 74 hadi 76, Yanga wanaitumia kwa kugongeana, lakini kama ilivyo kawaida wanakwenda kumalizia kwa shuti dhaifu kabisa la Haji Mwinyi. Kipa Barthez yuko chini baada ya kuumia ubavuni, anatibiwa
Dk 73, Ahly wanafanya shambulizi jingine kali, lakini Bossou anaingia na kuosha mpira 'kindava'
SUB Dk 73 upande wa Ahly Hossan Ahour anaingia nafasi ya Hossan Hgally ambaye ni nahodha

hadi Dk 60 na 71, Yanga wanaonekana kuchangamka hasa katikati ya uwanja, wanagongeana vizuri lakini mipango ya mwisho katika umaliziaji inaonekana kutokuwa na nguvu SUB Dk 68 Ahly wanamtoa Subh anaingia Waridi Suleyman Yanga nao wanamtoa Tambwe na kumuingiza Msuva
Yanga nao wa Dk 66, Ngoma anamchambua nahodha na Ahly na kuingia vizuri kabisa lakini mabeki wa Ahly wanaokoa na kuwa kona. Inachongwa  lakini haina madhara Dk 66, hatari kwenye lango la Yanga lakini mabeki wa Yanga wanaokoa Dk 65 bado mpira umepooza, Ahly wanaonekana wamewa "win" Yanga, kwani hawajafanya shambulizi kali katika kipindi cha pili huku wao wakionekana kufanya wanachotaka SUB Dk 62, Geofrey Mwashiuya anaingia kuchukua nafasi ya Boubacar Dk 61, Yanga wanaonekana kupoteza mipira mingi zaidi huku kiungo chao hasa cha ukabaji kinaonekana kutokuwa na uhakika  Dk 59 anapiga mpira huo wa Kamusoko lakini anabutua juuuuuu...!! Dk 58, Boubacary alikuwa akijaribu kuwatoka mabeki wa Ahly anaangushwa na kuwa faulo nje ya 18
Dk 56, Kaseke anampa Kamusoko pasi nzuri kabisa lakini anapiga mpira juuu. Hakuwa makini wakati anajiandaa kupiga mpira huo...

KADI Dk 54, Telela analambwa kadi ya njano kwa kumuangisha Abdallah Said. Bado Ahly wanaonekana kumiliki mpira zaidi Dk 52, bado inaonekana hakuna shambulizi kubwa ambalo wamefanya Yanga katika kipindi hiki ukilinganisha na Al Ahly Dk 49, bado Ahly wanaonekana kuwa bora kwa kujiamini zaidi huku Yanga wakionekana bado na hofu baada ya kupoteza mpira kila mara baada ya pasi mbili, tatu
DK 47, Ahly wanaonekana kuuthibiti mpira zaidi zaidi ya Yanga, huku Yanga wakipata mpira wanaipoteza mapema jambo ambalo si sahihi kwao walio nyumbani Dk 46, Zacharia anamchambua Mwinyi na kupiga shuti linalogonga mwamba, ilikuwa hatari kwelikweli MAPUMZIKO DAKIKA 1+ YA NYONGEZA  Dk 41 hadi 45, bado inaonekana Ahly kuwazidi ujanja Yanga, wanamiliki mpira katika eneo lao au kucheza taratibu
Dk 38 hadi 40, Ahly wanamiliki mpira muda wote lakini wanaonekana "kununua" muda kwani wanajua kubaki na mpira ndiyo ulinzi wao Dk 37, Ngoma anawahadaa mabeki wa Ahly na kupiga shuti lakini kipa Akram yuko makini anadaka vizuri kabisa Dk 34, hadi sasa Yanga wamefanya madhambi mara 5 na Ahly mara 4
KADI Dk 33, Kipa Akram analambwa kadi ya njano kwa kupoteza muda. Hii ni kadi ya kwanza katika mechi hii Dk 32, Yanga wanafanya shambulizi jingine safi kabisa, lakini Telela anashindwa kumalizia mpira wa mwisho, goal kick

Dk 28 hadi 30, Yanga wanaotea mara mbili kupitia Yondani aliyepanda na Ngoma. Hali inayoonyesha inabidi wajipange kuutegua mtego huo Dk 27, Said anamtoka Bossou na kupiga shuti la 'akili' lakini mpira unatoka kidogo nje ya lango la Yanga. Yanga lazima wawe makini kwa kuwa kadiri muda unavyokwenda, inaonekana Ahly ndiyo wanauthibiti zaidi mchezo
Dk 23 hadi 26, mpira unachezwa katikati zaidi na ilivyo ni opening game, kwani mashambulizi ni kwa zamu Dk 22, Yanga wanafanya shambulizi kubwa, krosi nyingine safi ya Boubacar lakini  anaokoa, mpira unamkuta Ngoma anapiga shuti dhaifu, kipa Shariff Akram anadaka kwa ulainiii Dk 21, Gamal anapiga kichwa safi akiunganisha kona lakini mpira unatoka nje kidogo. KIpa Mustapha anaonekana kukasirishwa na walinzi
GOOOOOOOOO Dk 19, krosi safi sana ya Boubacary, beki Ahmed Said wa Al Ahly anautumbukiza mpira wavuni yeye mwenyewe... Dk 16, Yanga wanagongeana vizuri, Kamusoko anampa pasi nzuri Abdul anapiga shuti kali lakini mpira unamgonga beki na kutoka nje, kona. Inachongwa na Boubacary lakini ni kona butuuu
Dk 12 hadi 14, Yanga wanaonekana kuchangamka lakini safu ya ulinzi ya Ahly iko makini sana na wamejaza watu zaidi ya watano GOOOOOOOOOO Dk 11, Amri Gamal anaipatia Yanga bao kwa kichwa baada ya kupiga mpira wa kichwa kutokana na faulo iliyowachanganya mabeki wa Yanga waliodhani angepiga shuti...
DK 10, Bossou anafanya madhambi karibu kabisa na lango la Yanga, faulo. Dk 5, Juma Abdul anapiga mpira wa adhabu, shuti kali lakini linaishia mikononi mwa kipa
Dk 3, Al Ahly wanafanya shambulizi la kwanza lakini Yanga wanakuwa wepesi kung'amua mbinu zao Dk 1, Ngoma anawatoka mabeki wa Ahly, lakini kabla hajapiga wanaokoa na kuwa kona, inapigwa na Boubacary, anaigonga Tambwe unatoka na kuwa goal Kick.

Mechi ndiyo imeanza na kila timu inaonekana iko makini.


KIKOSI CHA YANGA:
1. Ally Mustapha
2. Juma Abdul
3. Mwinyi Haji
4. Kelvin Yondani
5. Vicent Bossou
6. Thabani Kamusoko
7. Deus Kaseke
8. Salum Telela
9. Amissi Tambwe
10. Donald Ngoma
11. Yousouf Boubacary

BENCHI:
Deo Munishi
Oscar Joshua
Pato Ngonyani
Geofrey Mwahiuya
Simon Msuva
Paul Nonga


Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment