Nikikuuliza unapenda kipi kutoka kwa
mpenzi wako najua wengi watatoa majibu tofauti tofauti wapo watakao
sema, mcheshi, anamvuto napenda anavyotabasamu na vitu vingine kama
hivyo, LAKINI leo kupitia www.newspointtz.blogspot.com katika newspointtz Mahaba karibu uyatambue mambo matatu muhimu ili kumdatisha mwenza wako.
1.UZUNGUMZAJI WAKO
Unavyozungumza na mpenzi wako ni tofauti kabisa na navyozungumza na watu
wengine. Ni hatari sana kutumia lugha ya ukali ama isiyo ya kiungwana
kwa mpenzi wako. Unatakiwa kufahamu kwamba, mpenzi wako ni mtu muhimu
sana katika maisha yako hivyo unatakiwa kuwa makini pindi unapozungumza
naye.
Kuonesha kwamba wapo wasiojua mapenzi ni
nini, unamkuta mtu anamwita mpenzi wake majina kama vile mshamba, demu,
shembe na mengine mengine kama hayo. Mpenzi wako kweli umuite demu? Na
wale wengine kule mtaani utawaita nani?
Huo si ustaarabu na kamwe mapenzi yenu
hayawezi kushamiri kwa mtindo huo. Kuna wengine matusi hayawaishi
midomoni mwao. Kwa kufanya hivyo jua tu kwamba unamboa laazizi wako.
Aidha mapozi katika uzungumzaji wako ni miongoni mwa vitu vinavyoweza
kumdatisha
2.TABIA ZAKO
Huu ndio msingi imara wa uhusiano wa kimapenzi. Wapo wanawake ambao
ni wazuri na wenye kila sifa ya kuwa na wapenzi bora, lakini
kutokanana tabia zao chafu wamekuwa wakiachwa kila wanapoingia katika
uhusiano.
Nani atakupenda na kudiriki kuendelea
kuwa katika uhusiano na wewe kama tabia zako si nzuri? Wengi wetu
tunapenda kupata sifa ya kuwapata wapenzi ama wachumba wenye tabia nzuri
ili tuweze kusifiwa na marafiki zetu pamoja na wazazi.
Kwa maana hiyo basi, kuwa makini sana na
tabia ambazo unajua haziwezi kumvutia mpenzi wako ama jamii
inayowazunguka kama vile WIVU uliopitiliza kiasi cha kuwa kero, kutaka
makuu pamoja na tamaa zisizo na msingi.
Nimeweka wivu juu kutokana na ukweli
kwamba, kuna wanawake hata wakiwakuta wapenzi wamesimama ama kupigiwa
simu na mtu wa jinsia tofauti bila kujua ukweli wa mambo wanaanzisha
vurumai, huu ni ulimbukeni.
3. JINSI UNAVYOMRIDHISHA
Yote hayo hapo juu ni tisa, lakini kumi ni jinsi unavyoweza kumridhisha
mpenzi wako hasa mnapokuwa faragha mkipeana raha za dunia.
Hata kama una tabia nzuri na umbile la
kumvutia kiasi gani, kama huna utaalam na ujuzi wa kutosha katika kumpa
raha mpenzi wako hasa linapokuja suala la tendo la ndoa, lazima penzi
ama ndoa yako itakuwa na walakini.
Lakini kitu ambacho kimekuwa kikiwavutia
walio wengi waume kwa wanawake ni utundu na ubunifu wakati mnapokuwa
faragha. Kinachotakiwa ni kupeana kile roho inataka ili suala la
kusalitiana lisiwepo.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
Mambo matatu ya kumpagawisha mpenzi wako
Reviewed by Newspointtz
on
07:19:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment