NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

MGULULI:Kero ya Madawati sasa basi Kata ya Mahenge Ulanga

Afisa mtendaji Kata ya Mahenge Mjini Rajabu Hussen Mgululi
MAHENGE-ULANGA

Na.Timotheo Lupembe

Ofisi ya kata ya Mahenge Mjini imefanikiwa kuodoa kero ya Madawati 135 katika Shule mbili za Msingi na Moja ya Sekondari katika Kata hiyo.

Akizungumza na newspointtz.blogspot.com Ofisini kwake Afisa mtendaji kata ya Mahenge Mjini  Bwana Rajabu Mgululi amesema ofisi yake kushirikiana na wadau wa maendeleo wamehakikisha zoezi hilo linafanikiwa kwa haraka ili kuondoa kero hiyo kwa wanafunzi.

Aidha Bwana Mgululi ametaja Shule hizo ni Shule ya Msingi Mahenge Mjini Madawati 23,Shule ya Msingi Mahenge B Madawati 60 na shule ya Sekondari Mahenge 52 ambpo mpaka sasa jumla ya Madawati  68 kati ya 135 yamekamilika na kukabiziwa huku  Madawati 67  yakiendelea kutengenezwa.

Pia alisema upatikanaji wa pesa ni changamoto kubwa ambayo Ofisi ya Kata inapitia ili kutatua kero mbalimbali za kijamii na hilo wamelifanikisha na ongezo la pesa kutoka kwa wadau wa maendeleo ambao ni Wafanya Biashara

Hata hivyo Bwana Mgululi ametoa ushauri kwa wazazi kuwapeleka watoto wao Shuleni kwani kero ya upungufu wa Madawati Ofisi ya Kata kushirikiana na wadau wa maendeleo wameitatua kwa kiasi kikubwa


Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment