Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amemueleza Mkuu wa Idara ya Utumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Sigrifid Kaunala kuwa ni miongoni mwa watumishi watakaochunguzwa kutokana na kugundulika kuwepo kwa baadhi ya watumishi hewa waliopata mamilioni ya fedha kama mikopo kutoka taasisi za fedha.

Mongella
alitoa kauli hiyo jana wakati alipokuwa akizungumza na watumishi wa
Halmashauri ya Jiji hilo ambao pamoja na mambo mengine alitumia nafasi
hiyo kuzungumzia suala la watumishi hewa.
Alisema
baada ya uchunguzi wa uhakiki wa awamu ya pili wa watumishi hewa
uliofanywa na Serikali mkoani humo umebaini kuwepo kwa watumishi watano
(majina yao yanahifadhiwa) waliojipatia mikopo ya mamilioni ya fedha
kutoka taasisi za fedha hali inayoonesha baadhi ya mikopo hiyo
isingetolewa bila ya kibali cha waajiri wao.
“Mkuu
wa utumishi nasikia hata wewe unahusika kwenye sakata hili la watumishi
hewa, haiwezekani mambo haya yatokee na wewe usijue na wewe ni miongoni
mwa watu tunaowachunguza,” alisema Mongella.
Naye
Mwenyekiti wa Kamati ya Mkoa ya kuhakiki watumishi hewa, Waryoba Sanya
alisema kazi ya kuhakiki watumishi walioko kazini lilianza jana kwa
kuanza na uhakiki wa watumishi wote wa Ofisi Kuu ya Halmashauri ya Jiji
la Mwanza walioko kazini na kuwa lilikuwa linaendelea vizuri.
0 comments:
Post a Comment