Baraza
la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa kushirikiana na
Shirika la Kazi Duniani (ILO) wameanzisha mpango wa Ajira Yangu wenye
lengo la kuwainua vijana kiuchumi vijana.
Akizungumza
jana, Katibu wa Baraza hilo, Beng’i Issa alisema mpango huo unafanyika
kwa mfumo wa shindano kwa kuwashindanisha vijana nchi nzima kuanzia
miaka 18 hadi 35.
“Mpango
huu umebuniwa kwa ajili ya vijana kupata ujuzi wa kuanzisha na
kuendeleza biashara na kuwawezesha mitaji, ili waweze kuanza au
kuboresha biashara zao, na kutengeneza nafasi za ajira kwao wenyewe na
kwa vijana wengine pia,” alisema Issa .
Issa
alisema Ajira Yangu Business Plan Competition itahusisha vijana
wanaotaka kuanza biashara au wanaotaka kupanua na kuboresha biashara zao
bila kujali kiwango cha elimu.
Alisema
vijana hao wanatakiwa kuja na mipango rasmi ya biashara kwa ajili ya
mashindano katika sekta za kilimo na kilimo usindikaji, ikiwa ni pamoja
na viwanda, vyombo vya habari, masoko na mawasiliano, michezo, vifaa,
sanaa na utamaduni, utalii na burudani.
Alisema
mipango hiyo pia ilenge katika mazingira na utunzaji wa mazingira,
ikiwa ni pamoja na biashara ya kijamii, biashara inayohusu habari na
mawasiliano, teknolojia, ikiwa ni pamoja na usindikaji biashara.
Alisema
awamu ya kwanza ya mpango huo itawahusu vijana kujaza fomu ya ushiriki
zilizo kwenye tovuti za ILO na NEEC ambapo mwisho wa maombi utakuwa Mei 9
mwaka huu kuanzia jana.
Issa
alisema awamu ya pili itahusisha mafunzo ya siku moja ya kina ya
mipango ya biashara ambayo itawakutanisha vijana 25 watakaochaguliwa na
baadaye vijana hao watawasilisha mipango yao kwa majaji na wawekezaji na
hapo vijana 10 watapewa mitaji yenye jumla ya dola za Marekani 75,000
(zaidi ya Sh milioni 150) .
Mratibu
Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kazi (ILO), Dk Annamaria Kiaga,
alitaka vijana wengi kujitokeza kwani shirika lake lina mipango ya
baadaye ya kuinua vijana.
Mratibu
Mtendaji wa Mradi wa Maendeleo wa umoja wa Mtaifa,Anamarie Kiaga
katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),
Beng’i Issa akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) jijini
Daar es Salaam jana kuhusiana na Progrmu ya umoja wa mataifa kuhusu
Ajira kwa vijana. Kushoto ni Mratibu Mtendaji wa Mradi wa Maendeleo wa
umoja wa Mtaifa,Anamarie Kiaga.
0 comments:
Post a Comment