Hospitali ya Taifa Muhimbili MNH, na Serikali kupitia Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee na Watoto, wametoa msimamo kuhusu sintofahamu iliyowakumba wagonjwa wa sickle cell (Selimundu),
waliokuwa wakipatiwa matibabu kwenye hospitali hiyo kubwa kabisa hapa nchini.
Kauli ya MNH kuhusu tiba ya Selimundu
“Tunapenda umma uelewe kuwa huduma hii haijasitishwa na wala Hospitali haitasitisha utoaji wa huduma hiyo.” Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Profesa Lawrence M. Museru, amewaambia waandishi wa habari leo Aprili 25, 2016.
Hofu ya wagonjwa
Awali baadhi ya wazazi wa watoto wenye kuugua maradhi ya Selimundu, wakiongozwa na Bi.Yasmin Razak, wameonyesha hofu ya maisha ya watoto wao kufuatia taarifa kuwa jumla ya wagonjwa 6,000 waliokuwa wakipatiwa matibabu ya Selimundu hospitalini hapo chini ya mradi wa utafiti wa ugonjwa huo, “Welcome Trust.” Watarudishwa kwenye utaratibu wa matibabu chini ya muongozo wa Wizara ya Afya kwenye hospitali walikotoka, kwa vile mradi huo wa utafiti umemaliza kazi yake Machi 31, 2016.
Gharama za matibabu ya Selimundu
Ni kweli kwamba takribani miaka kumi kulikuwa na mradi uliokuwa ukifadhili matibabu pamoja na utafiti wa wagonjwa wa selimundu, Mradi huu kwa sababu ya utafiti ulihitaji wagonjwa wote wa selimundu kuja Muhimbili kwa ajili ya utafiti na tiba. Hivyo basi hali hii ilisababisha wagonjwa wengi wanaohitaji huduma ya selimundu kuja Hospitalini hapa licha ya kwamba mahitaji yao hayakuhitaji utalaamu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili,” amesema Profesa Mseru.
Naye Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Wizara ya Afya, Dkt.Doroth Gwajima, amewaondoa hofu wagonjwa kuhusu gharama za matibabu hayo ambapo alisema, muongozo wa serikali uko wazi, wazee na watoto watapatiwa matibabubure na wengine wanachangia kupitia bima ya afya na fedha taslim, hata hivyokwa wale ambao hawatakuwa na uwezo utaratibu wa kuwapatia matibabu upo.
Hofu ya wagonjwa
Kutokana na mazoea ya muda mrefu ya kupatiwa matibabu bure ya ugonjwa huo wa selimundu, na hasa ikizingatiwa hakuna tiba ya kuuponya kabisa ugonjwa huo, wagonjwa wamehoji watawezaje kumudu kulipia gharama hizo? Wazazi wa watoto wanaougua ugonjwa huo, wametmuomba Rais John Magufuli, kuingilia kati suala hilo ili kuokoa maisha ya wagonjwa hao ambao kwa asili ya ugonjwa wenyewe, mgonjwa hupata maumivumakali mwilini, mabadilikoya viungo, na wakati mwingine kupungukiwa damu mara kwa mara.
Kauli ya Mganga Mkuu wa jiji la Dar es Salaam
“Hospitali zote za Manispaa ya jiji la Dar es Salaam, na hata zile zilizopo mikoani na wilayani, zina uwezo wa kutoa huduma za ugonjwa wa Selimundu, na hata ikionekana kuwa mgonjwa anahitaji matibabu zaidi, rufaa huandaliwa na mgonjwa hupelekwa kwenye hospitali kubwa zaidi ili kupatiwa matibabu yanayofaa,” Dkt.Grace Magembe, Mganga Mkuu wa jiji la Dar es Salaam.
Bi.Yasmin
Razak, akiwa amembeba mtoto anayeugua maradhi ya Selimundu (Sickle
cell), wakati wa mkutano wa waandishi wa habari kwenye hoteli ya Serena
jijini Dar es Salaam. Mama huyu ambaye mwanaye pia anaugua ugonjwa huo,
lakini matibabu yake anapata nchini Uingereza, ameamua kusimama kidete
kutetea wagonjwa wa selimundu kuendelea kuhudumiwa Hospitali ya Taifa
Muhimbili, na kumuomba Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kuingilia kati
mpango wa kuwaondoa wagonjwa 6,000 hospitalini hapo na kuwapeleka kwenye
hospitali wanakotoka.
Bi.Getrude Thadeo kutoka Tabora, akiwa na mtoto wake wa miaka 13, Angela Romwadi, ambaye anaugua Selimundu.
0 comments:
Post a Comment