Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye amelihasa
jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) kujenga uzalendo ndani ya jeshi
letu kupitia michezo mbalimbali ndani ya jeshi hilo.
Waziri
Nape ameyasema hayo wakati wamakabidhiano ya Ulingo wa Kisasa wa Ngumi
kwa Jeshi hilo ili wautumie kwa ajili ya maandalizi mbalimbali ya mchezo
wa ngumi kwani Serikali imeona ni sehemu salama zaidi na nidhamu ya
kuutunza ipo na hata pale utapohitaji kakutumika kwingine uchukuliwe na
kurudishwa jeshini hapo kwani jeshi hilo limeleta heshima kubwa ya
michezo nchini na kulifanya Baraza la Michezo ya Majeshi (BAMMATA)
kuimarika zaidi.
“Jeshi
la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limekuwa na mchango mkubwa sana katika
michezo hapa nchini na limetuletea sifa kubwa sana kwetu na hivyo
hatukuwa na shaka tulipoletewa ombi la ulingo huu. Ulingo huu utumike
vyema na ulete heshima hapa nchini,”alisema Nape.
Aidha
Waziri Nape alitoa rai kwa jeshi hilo kurudisha michezo jeshini kwani
inajenga uzalendo na kuimarisha umoja,undugu na urafiki. Waziri huyo pia
alikazia kuwa wizara yake itaendelea kushirikiana na jeshi hilo katika
michezo mbalimbali nchini.
Na Daudi Manongi
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akizungumza
jambo na Mkuu wa Mafunzo na Operesheni jeshi la wananchi Tanzania
(JWTZ), Meja Jenerali Issa S. Nassoro wakati wamakabidhiano ya ulingo wa
Ngumi leo jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (wa pili
kushoto) akiwa na Mkuu wa Mafunzo na Operesheni jeshi la wananchi
Tanzania, Meja Jenerali Issa S. Nassoro (wa kwanza kushoto) wakati wa
makabidhiano ya Ulingo wa Ngumi uliotolewa na Wizara hiyo kwa jeshi la
wananchi Tanzania (JWTZ). Wengine pichani ni Brigedia Jenerali Martin
Busungu ambaye ni mkurugenzi wa michezo jeshini (wa pili kulia) na Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Bw.Alex Nkenyenge.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akimvisha
medali bondia wa jeshi kama moja ya ishara ya ufunguzi wa ulingo wa
ngumi waliopewa na wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ili
kuimarisha mchezo wa ngumi jeshini na nchini kwa ujumla kwani ulingo huo
utatumiwa na baraza la Michezo ya majeshi kujiimarisha katika mchezo
huo. Wengine pichani ni Mkuu wa Mafunzo na Operesheni JWTZ, Meja
Jenerali Issa S. Nassoro (wa kwanza kushoto).
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akimkabidhi
Mkuu wa Mafunzo na Operesheni JWTZ, Meja Jenerali Issa S. Nassoro
ulingo wa Ngumi wa kisasa ambao wizara ilipewa na Serikali ya China kwa
ajili ya maendeleo ya ngumi nchini. Wizara imeamua kuwapa jeshi kwa kuwa
ni sehemu salama na watakuwa na nidhamu ya kuutunza na pia ulingo huo
utaimarisha Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA). Wengine
pichani ni Brigedia Jenerali Martin Busungu ambaye ni mkurugenzi wa
michezo jeshini (wa kwanza kushoto) na Kaimu mkurugenzi Idara ya
Maendeleo ya Michezo wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw.
Alex Nkenyenge (wa kwanza kulia).
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akipiga gitaa
pamoja na bendi ya jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) wakati wa
makabidhiano ya Ulingo wa Ngumi uliotelewa na Wizara hiyo kwa jeshi hilo
leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Daudi Manongi – Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo (WHUSM).
0 comments:
Post a Comment