NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

NEC:Uchaguzi umeisha sasa tufanye kazi

 

Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imetoa hati za shukrani kwa wadau walioshiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa kutambua mchango wao.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi hati hizo mwenyekiti wa NEC Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema Tume inatambua mchango mkubwa uliotolewa na wadau wa uchaguzi kwani Tume peke yake isingeweza kufanya kazi hiyo.

Jaji Lubuva amesema uchaguzi umemalizika hivyo ni vema sasa wananchi kushikamana kwa pamoja kitaifa ili kuendelea kuijenga nchi kwa amani na upendo.

Waliokabidhiwa hati hizo ni vyama vyote vya siasa pamoja na wadau wengine ambao walishiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015

Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment