Mchezaji
wa zamani wa Brazil, Pele ametoa mawazo yake kuhusu nafasi ya nahodha
wa timu ya taifa ya Brazil, Neymar kuwa mchezaji bora wa dunia.
Akizungumza
na Gazzeta World, Pele alisema kuwa anaamini Neymar ana uwezo lakini
atakuwa mchezaji bora wa dunia baada ya miaka kadhaa kutokana na kuwa na
ushindani mkubwa kutoka kwa Messi na Ronaldo.
“Kwa
sasa mchezaji bora wa dunia ni Messi, na pia hata Ronaldo ni mchezaji
mzuri lakini kwa kipindi cha miaka miwili ijayo naamini Neymar atakuwa
mchezaji bora wa dunia, alisema Pele.
0 comments:
Post a Comment