Rais
John Magufuli amezua mjadala baada ya kuvamia tawi la CRDB (Holland
Branch), akiwa kwenye gari namba T 182 DFQ huku likiwa halina nembo ya
“Adamu na Hawa” wala bendera ya Rais.
Tukio
hilo lililochukuwa dakika 25, limetokea majira ya asubuhi jijijni Dar
es Salaam katika tawi hilo ambalo liko katika makutano ya barabara za
Ohio na Samora, bila kutarajiwa.
Mara
baada ya Rais Magufuli kufika katika eneo liliko tawi hilo, makutano ya
barabara hizo yalifungwa ndipo Rais aliposhuka kwenye gari na kuingia
ndani ya benki hiyo.
Wakati
akikaribia kuingia ndani ilibidi baadhi ya wateja waliyokuwa
wakijiandaa kuingia ndani ya benki hiyoi wazuiwe kuingia huku huduma
ikiendelea tu kwa wale ambao waliyokwishaingia.
Aidha,
baada ya kuingia ndani baadhi ya wateja wa tawi hilo na wananchi
wengine walibaki wakishangaa huku wengine wakijiuliza imekuwaje Rais
kuingia benki kwa sitaili ile. Baadhi ya wananchi walisema hawajaona
tukio kama lile kwa Marais wote waliyopita.
James
Charles, ambaye ni dereva wa taxi, alisema baadhi ya wananchi
waliyokuwa kwenye eneo hilo baada ya kuona ulinzi unaimarishwa
walishituka na mara wakamuona Rais Magufuli akishuka kwenye gari, hali
iliyowafanya wafikirie anakwenda kutembelea ofisi yake ya zamani.
“Lakini
kufumba na kufumbua tukamuona anaelekea kwenye benki ya CRDB,
tukajiuliza vipi rais leo kaamua kuwa kama mteja? Hata hivyo tujui kama
hiyo ilikuwa inawezekana. Lazima kutakuwa na kitu. Haiwezekani aende
akachukue fedha kwa utaratibu ule. Ngoja tusubiri tutasikia amefuata
nini,” alisema Charles.
Joyce
Godwin ambaye ni mwanafunzi wa chuo kimojawapo cha elimu ya juu alisema
kuja kwake kumewashtua wafanyakazi wa tawi la benki hiyo kwani
walidhani alikwenda pale kwa ajili ya kutumbua majipu.
“Mimi
wakati Rais Magufuli anaingia nilikuwepo ndani kwenye foleni nikisubiri
huduma. Kwa ujumla kila mmoja wetu alishituka lakini hatukujua
kilichomleta,” alisema.
Baada ya Rais Magufuli kumaliza kazi yake iliyompeleka alitoka na kuingia kwenye gari huku akiwapungia mkono wananchi.
Rais John Pombe Magufuli akiondoka katika benki ya CRDB, Tawi la Holland baada ya kumaliza shughuli iliyompeleka.
Rais John Pombe Magufuli akiwapungia wananchi mkono wakati akiondoka katika benki ya CRDB, Tawi la Holland.
0 comments:
Post a Comment