Mchezo mmoja wa Ligi Kuu ya Uingereza umeendelea usiku wa Jumatatu ambapo Stoke City ilikuwa mwenyeji wa Tottenham Hotspur katika uwanja wake wa nyumbani wa Britannia.

Mchezo huo umemalizika kwa wenyeji Stoke City kumaliza mchezo huo kwa kupokea kipigo kutoka kwa Totenham Hotspur cha goli 4-0, magoli ya Tottenham yakifungwa na Harry Kane aliyefunga magoli mawili dk. 9 na 71 na mengine mawili yakifungwa na Dele Alli dk. 67 na 82.

Baada ya matokeo hayo, Tottenham imefikisha alama 68 ikiwa nyuma kwa alama tano na viongozi wa ligi, Leicester City ambao wana alama 63, kwa upande wa Stoke City wao wamemesalia katika nafasi ya tisa ya msimamo wakiwa na alama 47.