Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha
Makatibu Tawala wapya kumi aliowateua tarehe 25 Aprili, 2016 na
kuwapangia vituo vyao vya kazi.
Makatibu
Tawala hao wameapishwa leo tarehe 27 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es
salaam na kisha wametia saini hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa
umma, zoezi lililoendeshwa na Kamishna wa maadili Sekreatieti ya Maadili
ya Viongozi wa Umma, Mheshimiwa Jaji Salome Kaganda na kushuhudiwa na
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
Makatibu Tawala walioapishwa ni;
- Arusha - Richard Kwitega
- Geita - Selestine Muhochi Gesimba
- Kagera - Armatus C. Msole
- Kilimanjaro - Eng. Aisha Amour
- Pwani - Zuberi Mhina Samataba
- Shinyanga - Albert Gabriel Msovela
- Singida - Dr. Angelina Mageni Lutambi
- Simiyu - Jumanne Abdallah Sagini
- Tabora - Dkt. Thea Medard Ntara
- Tanga - Eng. Zena Said
Makatibu
Tawala wengine wa Mikoa ambao hawakuapishwa leo, ni wale waliohamishwa
vituo vya kazi na wale waliobaki katika vituo vya kazi walivyokuwep,o
ambao tayari walishakula kiapo cha kuwa Katibu Tawala wa Mkoa.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaa
27 Aprili, 2016
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akimuapisha ndugu Albert Gabriel Msovela kuwa katibu Tawala wa Mkoa wa
Shinyanga Ikulu jijini Dar es salaam April 27,2016
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akimuapisha ndugu Amantius Casmiri Msole kuwa katibu Tawala wa Mkoa wa
Kagera Ikulu jijini Dar es salaam April 27,2016
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akimuapisha ndugu Angelina Mgeni Lutambi kuwa katibu Tawala wa Mkoa wa
Singida Ikulu jijini Dar es salaam April 27,2016
0 comments:
Post a Comment