Waziri
wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako,
amewatahadharisha kuwawajibisha maafisa elimu wa shule za msingi
watakaoshindwa kusimamia elimu na kusababisha wanafunzi wamalize shule
za msingi bila kujua kusoma na kuandika.
Prof.
Ndalichako amesema hayo Mjini Iringa katika mafunzo ya wakaguzi na
wadhibiti wa ubora wa elimu mashuleni kutoka wilaya 31 kutoka mikoa ya
Nyanda za Juu Kusini.
Prof.
Ndalichako amesema kuwa ni aibu kwa wanafunzi waliosoma miaka saba
darasani hawajui kusoma na kuandika wakati Wakaguzi na Wasimamizi wa
Elimu wapo katika maeneo husika na kuwataka wajitathimini kama
wanatekeleza wajibu wao ipasavyo.
Waziri
huyo pia amewataka wadhibiti hao wa elimu kufanya ukaguzi wa vitabu na
vifaa vya kufundishia vikiwa na ubora unaokubalika huku akiahidi
kuzingatia mahitaji ya walemavu katika shule za serikali.
Kwa
upande wao walimu pamoja na wadhibiti hao wa elimu wameiomba serikali
kushughulikia madai yao na kuboresha mazingira ya kufanyika kazi ikiwemo
pamoja na fungu la kutosha na kuendeshea ukaguzi wa elimu.
Mkuu
wa wilaya bwana Richard Kasesela akitoa salamu alisema " ni wakati
muafaka kubadili KKK iliyopo iliyo zoeleka sasa yaani KULA, KULALA na
KUCHEZA kuiirejesha kwenye maana halisi ya KUSOMA, KUANDIKA na KUHESABU.
Mkuu
wa mkoa Bi.Amina Masenza akimkaribisha Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi Dkt. Ndalichako,Bi Masenza alimuomba waziri wa Elimu kuhakikisha
Wahakiki ubora wanapewa kipaumbele katika kukuza elimu Tanzania.
Baadhi
ya waliohudhuria mafunzo kwa wakaguzi wa uhakiki ubora wa elimu
Tanzania yaliyofanyika katika chuo cha walimu Kleruu leo. Mafunzo hayo
yajumuisha mikoa ya Iringa, Njombe, Ruvuma, Katavi, Sumbawanga, Songwe
na Mbeya.
0 comments:
Post a Comment