NYOTA
wa sinema za Bongo, Issa Mussa ‘Cloud’ amefunga ndoa tena, lakini
safari hii ni kwa siri huko nchini Sweden na mwanamke aliyetajwa kwa
jina moja la Mina ambaye amekuwa akimposti kila kukicha mitandaoni kwa
kumuita pacha.
Chanzo kilicho karibu na staa huyo kililiambia gazeti hili kuwa, Cloud
amemfanyia mbaya mkewe, Cynthia kwa kuamua kuoa kwa siri wakati imani
yake inamruhusu kuwa muwazi.
Chanzo kilisema kuwa, awali Cloud alimwambia mkewe wa Bongo kuwa,
amepata mfadhili hivyo anakwenda nchini Comoro kupata matibabu ya moyo
ambao umekuwa ukimsumbua kwa muda mrefu, kumbe haikuwa hivyo bali
alikwenda Sweeden ambapo yupo na mwanamke huyu anaedaiwa kufanya kazi ya
uuguzi huko...mkwewe Cloud baada ya kusikia nyeti hizo kwa sasa amerudi
nyumbani kwao.....
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment