Diwani
wa Kata ya Kiwalani, Mussa Kafana (Cuf), ameibuka mshindi katika
uchaguzi wa Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, kwa kumbwaga mpinzani
wake kwa kura nne.
Uchaguzi
huo ulifanyika jana katika ukumbi wa Karimjee, baada ya madiwani wa
jiji hilo, ambao pia ni wajumbe wa Baraza la Halmashauri ya jiji hilo
kuapishwa.
Akitangaza
matokeo ya uchaguzi huo, Kaimu Mkurugenzi wa jiji hilo, Sarah Yohana
alisema, Kafana ameibuka mshindi kwa kura 10 huku mpinzani wake Mariam
Lulida (CCM) akipata kura sita.
“Kura zilizopigwa ni 16 na hakuna iliyoharibika. Namtangaza Mussa Kafana kuwa Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam,” alisema Yohana.
Awali
Meya wa jiji hilo, Isaya Mwita alisema, baraza hilo lina jukumu la
kuhakikisha linatekeleza majukumu yake ipasavyo na kila mjumbe kupitia
chama chake anapaswa kutoa mchango utakaoweza kulibadilisha Jiji la Dar
es Salaam.
Akizungumza
baada ya kutangazwa kuwa mshindi, Kafana aliwashukuru wajumbe wa baraza
hilo huku akiahidi kushirikiana nao bila kubagua itikadi za vyama vyao,
kwani wanafanya kazi kwa ajili ya wananchi na si vyama vyao.
Alisema kwa sasa vyama havina nafasi bali maendeleo ya wananchi wa jiji hilo ndio muhimu.
Naye
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Huduma za Sheria kutoka Ofisi ya Rais,
Tamisemi, Eustard Ngate, alisema, Halmashauri ya jiji hilo ilishawahi
kuvunjika mara mbili mwaka 1983 na mwaka 1996 kutokana na viongozi wake
kushindwa kuwajibika hivyo hawategemei hilo litokee
0 comments:
Post a Comment