Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa
unakutana kujaribu kufikiria mkakati wa kimataifa katika vita dhidi ya
dawa za kulevya hii ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha miongo
miwili ilyopita .
Maraisi hao wametoa mtazamo wao kuwa sera zilizopo zimeshindwa kulimaliza suala hilo na kutoa wito kwa mabadiliko ya sera na kuweka msisitizo zaidi katika masuala ya haki za binaadamu na masuala ya afya.
Barua hiyo imeeleza kuwa mamilioni ya watu wako magerezani, wamefungwa kwasababu ya dawa za kulevya,miongoni mwao ni masikini na wanatoka katika makabila madogo.
Ikumbukwe kwamba katika hotuba yake aliyoitoa mwezi uliopita, Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon alisema kwamba ni vyema kuhakikisha panakuwepo utokomezaji wa dawa za kulevya lakini pia ni muhimu kuwashirikisha walinda usalama, kada ya utawala na wataalamu wa afya ya umma.
Hii ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha miongo miwili ilyopita .
Kabla ya kikao siku tatu kuanza , barua ya wazi iliyosainiwa na zaidi ya watu elfu moja wakiwemo maraisi wastaafu wa Mexico,Colombia na Brazil wametoa wito wa mbinu huria zaidi katika kukabiliana na changamoto hiyo.
Maraisi hao wametoa mtazamo wao kuwa sera zilizopo zimeshindwa kulimaliza suala hilo na kutoa wito kwa mabadiliko ya sera na kuweka msisitizo zaidi katika masuala ya haki za binaadamu na masuala ya afya.
Barua hiyo imeeleza kuwa mamilioni ya watu wako magerezani, wamefungwa kwasababu ya dawa za kulevya,miongoni mwao ni masikini na wanatoka katika makabila madogo.
Ikumbukwe kwamba katika hotuba yake aliyoitoa mwezi uliopita, Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon alisema kwamba ni vyema kuhakikisha panakuwepo utokomezaji wa dawa za kulevya lakini pia ni muhimu kuwashirikisha walinda usalama, kada ya utawala na wataalamu wa afya ya umma.
chanzo>bbcswahili
0 comments:
Post a Comment