Ilikuwa ni rahisi sana kwangu kumshirikisha Chidi Benz – Alikiba
Alikiba amesema kuwa ilikuwa ni rahisi sana kwake kumpata Chidi Benz kwenye wimbo wake ‘Far Away.’
Staa huyo alifanikiwa kumshirikisha Chidi Benz kwenye wimbo huo ambapo kwa kipindi hicho nyimbo za Chidi zilikuwa zikifanya vizuri redioni na kwenye TV.
Akiongea kwenye Collabo ya Planet Bongo, inayoruka kupitia EA radio, Alikiba amesema, “Idea ya Far Away, ilitokea tu wakati nipo studio. Niliunganisha unganisha tu mistari ikatokea vile.
Ilikuwa rahisi sana kumpata Chidi Benz kwa sababu wote tulikuwa karibu sana na tulikuwa tunakaa sehemu moja. Nilimchukuwa tu nikampeleka studio kama nilivyomfanyia Dully Sykes,” alisema Kiba.
0 comments:
Post a Comment