Watumishi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, (TMA) wametakiwa kuachana na mfumo wa zamani wa kutumia makaratasi katika kuhifadhi taarifa zao muhimu na badala yake kuanza kutumia mfumo wa kisasa wa kieletroniki.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Pof. Makame Mbarawa jana
jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na wafanyakazi hao na kueleza
kuwa kwa kufanya hivyo kutasaidia kupunguza matumizi ya fedha za
kununulia karatasi.
“Katika
ofisi zenu nimeona kila mtu anakomputa ni jambo zuri hivyo zitumieni
katika kuhifadhi taarifa muhimu za taasisi yenu kwa mfumo wa
kieletroniki” alisema Mhe.Prof.Mbarawa.
Aliongeza
kwa kusema kuwa serikali imetumia fedha nyingi katika kujenga mkongo wa
taifa wa kuhifadhi taarifa muhimu hususani za serikali pamoja na
Taasisi zake hivyo ni budi waanze kuutumia mkongo huo kwa kuhifadhia
taarifa zao.
Pia
aliongeza kwa kuwataka watumishi kuwa waadilifu,wachapaka kazi
,wabunifu na kuwa na uwazi baina ya watendaji wa juu na watumishi wa
ngazi ya chini kwa kushirikiana na wafanyakazi wa mikoani .
“Watanzania
wanamatarajio mengi kutoka kwetu katika kukuza uchumi wa nchi hivyo ni
wajibu wetu kutimiza matarajio yao kwa kuwapatia mahitaji muhimu
ikiwemo miundo mbinu imara ya barabara, bandari ,shirika la ndege la
kisasa na utabiri wa hali ya hewa wenye uhakika ” alisema Mhe.Prof.Mbarawa.
Prof.Mbarawa
alitoa wito kwa kuwataka watumishi hao kufanya kazi kwa ushirikiano
kila mmmoja kujituma katika eneo lake la kazi ili kuleta matokeo
yaliyobora na hivyo kukuza uchumi wa nchi kwa kufikia uchumi wa kati.
0 comments:
Post a Comment