MAHENGE-ULANGA
Na.Timotheo Lupembe
Mama wajawazito Wilayani
Ulanga wametakiwa kuwahi kupata huduma katika kitengo cha wajawazito Hospitali
ya Wilaya ya Ulanga kwani huduma hizo hutolewa bila malipo
Hayo yamesemwa na Afisa
Muuguzi msaidizi kitengo cha wajawazito Hospitali ya Wilaya ya Ulanga Bi. Neema Baharia alipozungumza na newspointtz.blogspot.com
ofisini kwake na kuwataka wajawazito kufanya hivyo kwani huwasaidia kujua hali
ya mototo pindi yupo tumboni na kufahamu taratibu za kujifungua.
Aidha Bi.Baharia alisema licha ya Serikali kutoa huduma bure kwa
wajawazito katika Hospitali za Serikali na wao hutoa elimu kwa njia ya
vipeperushi lakini bado wanakumbana na changamoto ya uelewa mdogo kwa baadhi ya
wajawazito pindi wanapotoa elimu ya uzazi na maandalizi ya kujifungua.
Kwa upande wake mmoja kati
wajawazito Hospitalini hapo Bi. Hadija
Mshamu ameipongeza serikali kwa kutoa huduma bure kwa wajawazito za upimaji
na utoaji wa chanjo na dawa hali
inayowafanya wapate uraisi wa kujua hali zao na maendeleo ya mototo pindi yupo
tumboni.
0 comments:
Post a Comment