Wanafunzi 140,wa Shule ya Sekondari ya Mtakatifu Petro
iliyopo Manispaa ya Tabora, wamenusurika kifo baada ya mabweni mawili
kuteketea kwa moto wakati wakiwa madarasani, ambapo hakuna
kilichookolewa ndani kutokana na moto huo kushindikana kuzimwa, baada ya
gali la zimamoto kuzama eneo la shule hiyo.
Mkuu wa Shule hiyo inayomilikiwa na Kanisa Agrikana
Bw.Simon Peter Kyalla amesema kuwa, tukio hilo linawakumbusha machungu
kwani mwaka jana 2015 mabweni mawili moja la wavulana, na la wasichana
kwa nyakati tofauti yaliteketea kwa moto, na taarifa za tukio la sasa
hawajajua chanzo chake mpaka wafanye tathimini.
Kutuatia tukio hilo la mabweni kuwaka moto katika mazingira
ya kutatanisha tena mchana kweupe, Mkuu wa Wilaya ya Tabora mjini Bw,
Suleimani Kumchaya ameamua kuifunga shule hiyo kwa muda usiojulikana
akidai kuwa, mpaka viongozi wa taasisisi hiyo wajihoji, si kilasiku ni
tatizo la umeme.
Kwa upande wake,Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto mkoani Tabora
Bw.Kondo Mohamed ameasema kuwa, changamoto iliyowakumba ni mvua
zinazoendelea kunyesha mkoani Tabora pamoja na miundombinu duni ya
barabara ambayo imesababisha gali lenye maji kuzama.
Source:ITV
0 comments:
Post a Comment