Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu, Ajira, kazi na watu
wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama amewatembelea wananchi waliopatwa na
majanga ya kuangukiwa na kifusi eneo la Kawe na kuwapa mkono wa pole.
Akiongea
na moja ya familia zilizopatwa na maafa hayo Mhe. Jenista Mhagama
amesema kuwa Serikali imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya tukio
hilo na kwa vifo vilivyojitokeza na kuahidi kutoa ushirikiano kwa
familia ya wafiwa na waathirika wa tukio hilo.
“Ndugu
zangu tumekuja kushirikiana nayi kwenye msiba huu mzito, ambao wenzetu
wamepoteza karibu familia nzima kutokana na haya maafa, poleni sana kwa
msiba na Serikali ipo pamoja nayi katika kipindi hiki kigumu,” alisema
Mhe Jenista.
Mhe.
Jenista Mhagama ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano wakati
Serikali inapokuja kwa ajili ya kujadili jinsi ya kutatua mambo
yanayowezesha kuhatarisha maisha yao hasa, tatizo la makazi yaliyopo
mabondeni kwa ajili ya usalama wao na familia zao katika kuzingatia
suala la mipango miji ili kuepukana na majanga kama haya.
Aidha
kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Raymond Mushi
amesema kwa upande wake amesikitishwa na tukio hilo na kuongeza kuwa
Wilaya imejipanga kwa kushirikiana na kamati ya maafa ya Wilaya na Idara
ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu ili kuendelea kuangalia ni kwa namna
gani wataweza kuwasaidia wananchi waliobaki katika maeneo hayo.
Akitoa
shukrani kwa niaba ya familia ya wafiwa Bi. Gaudencia Deogratius ambaye
amepoteza mume na watoto wawili ameishukuru Serikali kwa faraja
aliyopata kutoka kwa Waziri na hakutegemea kupata ugeni huo na ameiomba
Serikali kuwasaidia wale waliopo mabondeni ili kuepusha majanga mengine
zaidi kutokea.
Tukio
la hili la nyumba kuangukiwa na kifusi katika eneo la Kawe Jijini Dar
es Salaam lilitokea April 7 mwaka huu na kusababisha vifo vya watu
watano wa familia moja.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye
Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagamaakitoa ubani kwa Gaudensia
Deogratius aliyefiwa na watoto wawili na mume baada ya kufunikwa na
kifusi Kawe Ukwamani Dar Es Salaam.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu)
Mhe. Jenista Mhagama akitoa mkono wa pole kwa mama wa marehemu Ephrahim
Mangule (aliyefariki kwa kuangukiwa na kifusi Kawe) wakati wa msiba huo
Kinondoni Dar es Salaam tarehe 9 Aprili, 2016
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu)
Mhe. Jenista Mhagamaakitoa salamu za pole kwa wafiwa waliopotelewa na
ndugu 3 baada ya mvua zilizonyesha Aprili 7, 2016 na kuangukiwa na
nyumba Kawe Dar es Salaam kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni
Mhe. Raymond Mushi.
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Raymond Mushi akizungumza na moja ya
familia ya wafiwa walioangukiwa na kifusi Kawe Dar es Salaam
wakati Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu
wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipowatembelea tarehe 9, Aprili,
2016.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu)
Mhe. Jenista Mhagama akiangalia chumba kilichoangukiwa na kifusi baada
ya mvua kubwa zilizonyesha Aprili 7, 2016 na kuua watu 5 wa familia moja
Kawe Dar es Salaam. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)
0 comments:
Post a Comment