Waziri wa Mambo ya Nje,
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt.
Augustine Mahiga amekutana na Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Masalia
ya kesi za Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (Mechanism for International
Criminal Tribunals-(MICT).
|
Waziri
wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,
Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Rais wa Mahakama ya
Kimataifa ya Masalia ya kesi za Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (Mechanism
for International Criminal Tribunals-(MICT) inayojengwa katika eneo la
Lakilaki jijini Arusha, Mhe. Theodor Meron. Rais huyo alifika Wizarani
kwa ajili ya kujitambulisha kwa Mhe. Waziri, kumweleza maendeleo ya
ujenzi wa Mahakama hiyo pamoja na kuishukuru Serikali ya Tanzania kwa
ushirikiano na mchango mkubwa inaotoa katika kufanikisha ujenzi huo. Pia
aliipongeza Tanzania kwa kuwa mstari wa mbele katika kusimamia utawala
wa sheria na haki. |
|
Sehemu ya ujumbe uliofuatana na Mhe. Meron, Rais wa MICT. |
|
Picha ya pamoja. |
|
Mhe. Mahiga na Mhe. Meron |
|
Mhe. Mahiga akiagana na Mhe. Meron |
|
………..Mkutano wa Waziri na Mwendesha Mashitaka wa MICT.
|
Waziri
wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,
Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Mwendesha Mashtaka wa
Mahakama ya Kimataifa ya Masalia ya kesi za Mauaji ya Kimbari ya Rwanda
(Mechanism for International Criminal Tribunals- (MICT), Mhe. Dkt.Serge
Bremmertz. Katika mazungumzo yao Mwendesha Mashtaka huyo aliipongeza
Tanzania kwa mchango wake mkubwa wa kuridhia taasisi za Umoja wa Mataifa
zinazosimamia sheria kujengwa nchini na kuielezea Arusha kama makao
makuu ya kimataifa ya haki kwa Ukanda wa Afrika. Pia aliahidi
ushirikiano hususan katika kuwajengea uwezo wataalam wa masuala ya
sheria za kimataifa hapa nchini. |
|
Seheme ya Wajumbe waliofuatana na Mwendesha Mashtaka wa MICT. |
|
Mazungumzo
yakiendelea. Kushoto kwa Mhe. Mahiga ni Bw. Elisha Suku, Kaimu
Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje,
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa. |
|
Mhe. Dkt. Mahiga akiagana na Mwendesha Mashtaka wa MICT, Dkt. Bremmertz. |
|
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia
Facebook
,
Twitter na
Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
0 comments:
Post a Comment