Waziri
wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako,
amewataka walimu na maafisa elimu kusimamia vyema majukumu yao na
kuhakikisha utoaji elimu bora kwa wanafunzi ili kupata wataalamu
watakaolisaidia taifa.
Waziri
Ndalichako, ameyasema hayo Jijini Arusha, alipokutana na wakuu wa
shule,maafisa elimu na watendaji wakuu wa idara za elimu ambapo
amesisitiza nidhamu ili kusaidia matokea mazuri na ya haraka ya
kuboresha elimu nchini.
Waziri
Ndalichako, amesema kuwa wataalamu mbalimbali ambao wanahitajia katika
idara mbalimbali katika kukuza maendeleo wote wanahitaji zaidi mchango
wa sekta ya elimu katika kuwapata wataalamu hao.
Aidha
katika ziara aliyoifanya katika mkoa huo wa Arusha, Waziri Ndalichako,
ametoa ufafanuzi zaidi wa sera ya elimu bure ambapo amesema kuwa wazazi
bado wanajukumu la kushirikiana na serikali katika kuwasadia watoto
kupata elimu bora.
Prof.
Ndalichako amesema serikali haijawazuia wananchi wanaotaka kuchangia
sekta ya elimu kutokana na changamoto zilizopo lakini haiko tayari kuona
mwanafunzi anarudishwa nyumbani kwa sababu ya michango ya aina hiyo.
0 comments:
Post a Comment