ligi kuu England imeendelea kwa
michezo mitatu kupigwa huku timu za West Ham, Liverpool,Man United
wakishinda michezo yao. Wagonga nyundo wa West Ham wameibuka na ushindi
wa maboa 3-1 dhidi ya Watford, mshambuliaji Andy Carrol, akifunga goli
la kwanza dakika ya 11 kisha kiungo Mark Noble akifunga mabao mengine
mawili kwa mikwaju ya penati.
Liverpool wakashinda dabi yao kwa kuwachapa Everton kwa mabao 4-0, mabao ya majogoo hao yakifungwa na Divock Origi,Mamadou Sakho,Daniel Sturridge,Philippe Coutinho.
Nao mashetani wekundu wa Man United wakaibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Crystal Palace, beki Damien Delaney alianza kuipa Man United goli la kuongoza baada ya kujifunga kisha beki wa kiitaliano Matteo Darmian akaongeza bao la pili na kuipa timu yake alama tatu muhimu.
0 comments:
Post a Comment