Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni
Dar es Salaam, Iddi Azani kupitia wakili wake Abubakari Salim amemuomba
Jaji Chochi wa mahakama katika Mahakam ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini
hapa, kufuta shauri la kesi yake aliyokuwa amemshitaki Maulidi Mtulia
(CUF) ambaye ndiye Mbunge wa sasa wa jimbo hilo kwa kile alichokuwa
akidai kuwa mbunge huyo hakushinda kihalali katika Uchaguzi Mkuu 2015.
Awali akiwasilisha ombi hilo wakili wa
Iddi Azani alisema wamefikiria maslahi mapana ya wananchi wa jimbo hilo
na hawakuona sababu ya kuendelea na kesi hiyo.
Majibu ya Hakimu Chochi kutoka Mahakama Kuu “Mahakama
hii haina nia wala sababu ya kulazimisha kuendelea kwa kesi hiyo, na
hivyo kwa mujibu wa kifungu cha 30, sheria ya mwenendo wa madai ya 33,
upande unaoshinda ndio unaostahili kupewa gharama, kwa hiyo nimeruhusu
shauri hili namba 3/2015 liondolewe mahakamani kuhusu gharama mtaelewana
wenyewe”.
Kwa upande wake Mbunge Mtulia amesema
amefurahia uamuzi wa Iddi Azani kwa kutambua umuhimu wa wananchi wa
Kinondoni, lakini pia ameeleza kufurahishwa na kitendo cha mahakama
kutenda haki.
Katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba
mwaka jana Maulidi Mtulia kupitia tiketi ya CUF alitangazwa kuwa Mbunge
halali wa Jimbo la Kinondoni kwa kupata kura 67,300 dhidi ya Iddi Azani
(CCM) aliyepata kura 65,700.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
IDDI AZANI (CCM) AJIONDOA KESI YA UBUNGE MAHAKAMANI
Reviewed by Newspointtz
on
16:04:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment