NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

NGEGE YA EGYPT YATHIBITIKA KUPATA AJALI

EGYPT 1KIDANGA ALLY

Ndege moja aina ya Airbus A320 ya Shirika la Ndege la Misri la EgyptAir, iliyokuwa ikitoka Mji Mkuu wa Ufaransa Paris hadi Cairo, imeripotiwa kupoteza mwelekeo na kupata ajali mapema leo asubuhi ikiwa na abiria 59 na wahudumu kumi, Maafisa wa Anga wa Misri wamesema.

Hata hivyo Waziri Mkuu wa nchi hiyo Sherif Ismail amesema bado mapema kutolea ufafanuzi wa ndege hiyo kama ni suala la kiufundi au shambulizi la kigaidi lililopelekea ndege hiyo kupata ajali.

EGYPTMapema mwaka huu ndege moja ya Shirika la Ndege la EgyptAir iliripotiwa kutekwa nyara na kulazimishwa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Larnaca Kusini mwa Pwani ya Taifa la Cyprus.

Ndege hiyo MS181,airbus A320 ilikuwa imebeba abiria 81 kutoka Alexandria kuelekea Cairo ilitekwa nyara na mwanaume mmoja aliyekuwa abiria wa ndege hiyo na kutishia kujilipua.

Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment