NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Itambue bifu nzito kati ya vanessa mdee na shilole

Divas wa Bongo Flava, Vanessa Mdee na Shilole wameingia kwenye bifu zito Bado kisa na mkasa hakijabainika wazi lakini ni Shishi ndiye aliyeanza kumtupia maneno Vee Money kwenye Instagram. Kuna uwezekano mkubwa wawili hao walizinguana nyuma ya pazia kabla ya kuamua kuumwaga ubuyu mtandaoni. “Vee Jipange sana mwenzio Igunga niliaga sijaletwa kwa kubebwa kwenye lori, nimekuja na mbio za mwenge,” aliandika Shilole kwenye post ya Instagram ambayo imefutwa tayari. “We si wa magorofani na kiingereza chako cha kuunga, mi ndio mtoto wa mbwa sasa maninaa,” aliongeza Shilole. Vanessa hakukaa kimya, alimjibu Shishi kwa post ambayo aliifuta muda mfupi baadaye. Akipost picha ya Shishi, Vee aliandika: Nikupe Kickiii ujulikane au sio? Kila siku twanyamaza ndio mtugaraze. Sit the f*ck down. Mimi sio wale uliowazoea. Ps: You ain’t worth this post inashushwa sasa hivi #MessageSent. Haijashia hapo. Shilole amepost video akimpa ujumbe mwingine mkali zaidi muimbaji huyo wa ‘Niroge.’
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment