Katika miaka 14 iliyopita hakuna mwanasoka aliyeingiza fedha nyingi zaidi ya Cristiano Ronaldo
Wakati Real Madrid wakitajwa kuwa kuwa klabu ya soka yenye thamani zaidi duniani, huku Manchester United wakitajwa kuwa klabu iliyotengeneza faida kubwa zaidi kwa mwaka uliopita, pia imetolewa listi ya wachezaji waliotengeneza fedha nyingi zaidi mwaka jana.
Cristiano Ronaldo ametajwa kuwa mwanasoka aliyetengeneza fedha nyingi duniani na pia mwanamichezo ambaye bafo anacheza ambaye amelipwa fedha nyingi zaidi – kwa mujibu wa jarida la masuala ya fedha la kimarekani Forbes.
Mshambuliaji huyo wa Real Madrid ameripotiwa kuwa alilipwa kiasi cha $82 million (£56.7m), huku mapato ya mshahara ni kiasi cha $53m (£36.7m) na $29m (£20m) ikitokana na matangazo ya biashara.
Nahodha hiyo wa Ureno, ambaye aliweka rekodi ya kuwa mchezaji ghali zaidi wakati aliposajiliwa kutoka Manchester United kwenda Real Madrid kwa ada ya uhamisho wa paundi millioni 80 mnamo mwaka 2009, alisainj mkataba mpya na Real Madrid mwaka 2013.
Forbes, imemtangaza Ronaldo kuwa mwanamichezo anayelipwa fedha nyingi kuliko yoyote duniani kwa sasa.
Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi, mshindi wa tuzo ya 2015 FIFA Ballon d’Or, ameshika nafasi ya lili akitengeneza kiasi cha $77m (£53.3m), kiasi cha $51m (£35.3m) kikitokana na mshahara na kiasi cha $26m (£18m) kikitokana na matangazo ya biashara. Nahodha huyu wa Argentina alisaini mkataba mpya na Barca mwaka 2014.
Forbes imeripoti kwamba Ronaldo ametengeneza kiasi cha $550m (£380.9m) katika kipinfi cha miaka yake 14 ya kucheza soka la ushindani, kuanzia Sporting Lisbob, wakati Messi ambahe maisha yake yote ameitumikia Barcelona ametengeneza kiasi cha $450m (£311.5m) ndani ya miaka 11.
Mcheza basketball Kobe Bryant, ambaye alistaafu mwishoni mwa mwezi uliopita, ndio mwanamichezo pekee ambaye ametengeneza fedha nyingi kuliko Ronaldo kwa ujumla – akitengeneza kiasi cha $680m (£470.8m) katika miaka 17 ya kucheza NBA.
Ronaldo na Messi, ambao wamekuwa washindi wa tuzo ya Ballon D’or tangu Ricardo Kaka aliposhinda tuzo hiyo mwaka 2007, wamemuacha mbali anayeshika nafasi ya 3, Zlatan Ibrahimovic.
Nahodha wa Sweden, mwenye umri wa miaka 34, ameingiza kiasi cha $37m (£25.6m) kupitia mshahara wake na PSG, huku $7m (£4.84m) zikitokana na mikataba wa biashara.
Mshambuliaji wa kibrazil Neymar ameshika nafasi ya 4, akiingiza kiasi cha $36m sawa na £24.9.
Forbes wameripoti kwamba Neymar ndio mchezaji ambaye ametengeneza fedha nyingi zaidi kupitia matangazo ya biashara – kiasi cha $22million kuliko mapato ya mshahara wake $14millioni.
Listi kamili ya wachezaji waliotengeneza fedha nyingi 2015:
1 Cristiano Ronaldo (Real Madrid): $82m (£56.7m)
2 Lionel Messi (Barcelona): $77m (£53.3m)
3 Zlatan Ibrahimovic (Paris Saint-Germain): $37m (£25.6m)
4 Neymar (Barcelona): $36m (£24.9m)
5 Gareth Bale (Real Madrid): $34m (£23.5m)
0 comments:
Post a Comment