NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Listi ya vilabu tajiri duniani, Madrid, Barca zaongoza, Man Utd yaongoza kwa kuingiza faida kubwa


Mapato makubwa ya fedha zinazotokana na mauzo ya haki za matangazo ya TV , mauzo jezi na mapato ya udhamini wa jezi, wadhamini na ushiriki wa Champions league umeendelea kuzipa uthamani mkubwa vilabu vya soka duniani.
 
  Matokeo yake, wawekezaji ambao waliwekeza kwenye soka katika kipindi cha mika 10 iliyopita sasa wanavuna mapato makubwa hasa katika timu za England.
UEFA imeongeza malipo katika Champions League kwa asilimia 50% kwa miaka 3 kuanzia msimu wa 2015-16. Fainali ya mwaka huu, itakayochezwa San Siro jijini Milan, Italy, baina ya vilabu vya Spain, Real Madrid vs Atletico, kila timu itapata kiasi cha $100 million.
Mapato ya Champions League msimu uliopita

Vilabu 20 ambavyo vinaongoza kwa uthamani vina thamani ya wastani wa $1.44 billion, ongezeko la 24% kuliko ilivyokuwa miaka 20 iliyopita. Malipo makubwa ya dili za TV, kama mkataba wa miaka wa miaka 3 wenye thamani ya $7.9 billion baina ya English Premier Keague na Sky Sports na BTSport ambao unaanza msimu wa 2016/17, na dili nyingine za udhamini wa jezi, mfano ukiwa mkataba wenye thamani ya $130m kwa mwaka baina ya Manchester United na Adidas.    Timu yenye thamani kubwa ya soka kwa mwaka wa nne mfululizo ni Real Madrid wakiwa na thamani ya $3.65 billion, ongezeko la 12% la thamani waliyokuwa nayo mwaka uliopita.
 Wanaowafuatia ni FC Barcelona ambao wana thamani ya $3.55 billion, ongezeko la 12% la thamani kutoka msimu uliopita.
 Barcelona huenda wakawapita wapinzani wao kutokana na mkataba wa $400 million la utengenezaji upya uwanja wao wa Camp Nou, ambao unategemea kukamilika ndani ya miaka mitano.
  Timu ya 3 kwa thamani kubwa ni Manchester United, klabu ambayo ipo kwenye soko la hisa. Forbes wanaitaja kuwa na thamani ya $3.32billion, ongezeko la asilimia 7 la thamani kutoka mwaka jana. Man United wametengeneza faida ya $190m kwa msimu wa 2014-15, kwenye listi  hii Man United ndio timu iliyoingiza faida kubwa kwa upande wa soka lakini wapo nyuma ya  Dallas Cowboys ($270 million) na New England Patriots ($195 million) kiujumla.
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment