NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe azungumza baada ya sakata la wanafunzi 7000 waliofukuzwa UDOM


 Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ambaye pia ni Mbunge wa Hai Freeman Mbowe amesema kwamba kambi rasmi ya upinzani itajadili hoja ya kutokuwa na imani na Naibu Spika Tulia Ackson kwa uendeshaji wake wa bunge ambao kambi hiyo hairidhiki

Mbowe ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutolewa nje kwa wabunge wa kambi rasmi ya upinzani kwa kutotii kiti cha spika kuhusu hoja ya wanafunzi zaidi ya 7000 kutoka chuo kikuu cha UDOM kusimamishwa masomo na kutakiwa kurudi makwao ndani ya saa 24 hadi hapo serikali itakapo tatua tatizo la walimu wa kuwafundisha baada ya waliopo kugoma.

Naibu Spika ametutaka wabunge wote wa kambi ya upinzani kutoka nje ya Bunge baada ya kushinikiza kiti kisimamie taratibu za sheria na kanuni za kuongoza bunge kwa kuwa hoja iliyoahirisha bunge asubuhi ni suala la wanafunzi wa UDOM ambapo kamati ya uongozi iliitwa ili kwenda kufanya uamuzi wa kumshauri spika ili bunge limalizie hoja.

''Si kanuni za Bunge hoja kujadiliwa na kuishia katikati, ikaja hoja nyingine ikakamilishwa na ile hoja ya awali ikarejeshwa tena, kwa muda wote nilioishi bungeni huu ni uamuzi wa kituko kuliko ambavyo niliwahi kuona''- Amesema Mbowe.

''Tumeona mara kwa mara bunge linavurujika, mienendo ya bunge inavurugika, maamuzi ya bunge yanapuuzwa hivyo ni pendekezo katika ajenda zetu ya kwanza tujadili agenda ya kutokuwa na imani naye na siku ambayo ataongoza kikao cha bunge sisi tutatoka nje''-Amesema Mbowe.
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment