Chama
cha Watanzania Waliosoma China kwa kiingereza China Alumni Association
of Tanzania (CAAT) kinapenda kukukaribisha katika sherehe ya maadhimisho
ya miaka 6 (2010-2016) tokea kilipozaliwa.
Sherehe
hiyo itafanyika katika ukumbi wa Cardinal Laurian Rugambwa Social
Centre pembezoni mwa kanisa la Mtakatifu Peter (St Peter), Oysterbay
Ijumaa ya tarehe 20-May-2016 kuanzia saa 8 alasiri.
Sherehe hiyo itahudhuriwa na viongozi wakubwa kutoka serikalini na baadhi ya wageni kutoka ubalozi wa China.
Pamoja
na burudani mbalimbali, maadhimisho hayo yatakuwa na hotuba kutoka
viongozi wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na viongozi wa
ubalozi wa Jamhuri ya watu wa China.
Kwenye
sherehe hiyo pia utafanyika uzinduzi wa tovuti (website) ya CAAT. Baada
ya chakula cha pamoja cha jioni, vilevile kutakuwa na fursa ya
wafanyabiashara, wajasiliamali na wafanyakazi waajiriwa kuonyesha bidhaa
au matangazo ya bidhaa au huduma wanazotoa.
Dhima kuu ya tukio hilo ni:
•Utambulisho
wa jumuia ya CAAT ambayo inajumuisha wataalam wa taaluma mbalimbali
waliohitimu mafunzo yao katika Jamhuri ya Watu wa China
•Kubaini na Kuainisha fursa zinazopatikana Tanzania na China kupitia CAAT
•Maonyesho ya bidhaa na huduma mbalimbali za biashara za wanajumuia.
Wote mliopata kusoma China mnakaribishwa. Hakutakuwa na kiingilio.
Unaweza
kushiriki kwa kuthibitisha uwepo wako kwa kupiga simu kwa Katibu
Mtendaji wa CAAT kwa kupitia 0783-992020 au 0715-200090 au
emailgsoreku@yahoo.com
Asante
George Oreku
Katibu Mkuu
Chama cha Watanzania Waliosoma China (China Alumni Association of Tanzania)
05-May-2015
0 comments:
Post a Comment