SPIKA
wa Bunge, Job Ndugai amempa siku tatu Mbunge wa Viti Maalumu, Susan
Lyimo (Chadema) awasilishe mbele ya Kamati ya Maadili ya Bunge, maelezo
ya utetezi dhidi ya madai aliyotoa bungeni kuhusu Serikali kununua
magari ya washawasha 777.
Ndugai
alitoa amri hiyo kutokana na mwongozo ulioombwa na Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yussuf Masauni juzi akitaka Lyimo
athibitishe au afute kauli yake juu ya madai hayo wakati serikali
imenunua magari 32.
“Hata
kwa akili ya kawaida haiwezekani Serikali ikaagiza magari yote hayo 777
ya washawasha. Ninachokumbuka mimi Waziri huyu aliwahi kusema hapa
bungeni kuwa magari hayo 777 ni idadi ya magari yote ya aina mbalimbali
yaliyonunuliwa kwa ajili ya matumizi ya polisi,” alisisitiza Ndugai.
“Sasa
nakutaka uniandikie rasmi majibu vizuri kuhusu kauli yako hii, nakupa
siku tatu uwe umeniletea na baadaye nitaipeleka taarifa yako kwa Kamati
ya Maadili ya Bunge, ili kujadili suala hili kwa mapana,”alisisitiza Ndugai.
Awali
mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu, Ndugai
alimpatia mbunge huyo nafasi ya ama kufuta kauli yake hiyo au
aithibitishe kabla ya hatua za kikanuni za Bunge hazijachukuliwa dhidi
yake.
Lyimo
alikataa kufuta kauli hiyo na kudai kuwa anao uthibitisho juu ya idadi
hiyo ya magari aliyoitamka na kusisitiza kuwa amenukuu taarifa za idadi
hiyo kupitia taarifa iliyotolewa na mtandao wa Jamii forum pamoja na
taarifa za Hansad za Bunge.
“Mheshimiwa
Spika mimi ni mtu mzima siwezi kwenda kwa hisia za watu, ni kweli jana
niliombewa mwongozo bahati mbaya sikuwepo ndani ya Bunge. Nathibitisha
kauli yangu na wala siifuti kwa kuwa nina uhakika na idadi ya magari
niliyoisema,” alisisitiza mbunge huyo.
Alisema
kwa mujibu wa Kanuni ya 63 (2) ya Bunge, mbunge hatasema uongo endapo
chochote atakachokisema ndani ya Bunge atakuwa amekirejea kwenye chombo
cha habari au taarifa za Bunge.
0 comments:
Post a Comment