KIKOSI CHA NDANDA |
Mashabiki
Ndanda FC wameeleza kuchukizwa na kitendo cha baadhi ya viongozi wa
klabu yao kukubaliana na viongozi wa Yanga, mechi yao ichezwe Dar es
Salaam badala ya Mtwara.
Mashabiki wapatao 126 waliotuma ujumbe mfupi kupitia SMS, ujumbe Facebook pia, wameonekana kukerwa.
Ingawa wako wenye msimamo wa kati ambao wanasema wangeelezwa lingekuwa jambo zuri, lakini kutoshirikishwa, ndiko kuna waudhi.
Kwa asilimia kama 15 hadi 25, wao wamezungumzia uzalendo kwamba Yanga wanashiriki michuano ya kimataifa ni vizuri kuwapa nafasi.
Waliobaki
ambao ni asilimia kubwa zaidi wanasisitiza hilo si jambo jema kwa kuwa
mashabiki wa Ndanda wangependa kuiona Ndanda ikicheza dhidi ya Yanga
pale Nangwanda.
“Hivi timu inahamishwa vipi, sasa watu wa Mtwara ambao tumeiunga mkono hii timu, tunawaona vipi Yanga,” alisema Abdul Msalamu.
“Siamini
kama viongozi wa Ndanda wanaweza kuwa na maamuzi ya kijinga kama haya,
kwa hiyo Mtwara nzima tusafiri kwenda Dar? alisema Mwafungo Joseph.
“Viongozi hawakutafakari, Ndanda imegeuka kuwa tawi la Yanga,” alisema Salum (huyu kajitambulisha kwa jina moja tu).
“Jamani
Ndanda tumekuwa nayo kwenye shida, leo kwenye shida za Yanga
imetukimbia,” alisema Monica Betram aliyejiita kwa jina la utani,
Mwanamtwara.
Hata
hivyo, uongozi wa Ndanda umesisitiza umefanya hivyo kwa sababu ya
uzalendo maana Yanga inashiriki michuano ya kimataifa na inaliwakilisha
taifa hivyo ilikuwa vigumu kusafiri hadi Mtwara, icheze halafu irudi Dar
es Salaam na kwenda kucheza tena Angola.
Lakini
uongozi huo umesisitiza, Yanga wamekuwa ni rafiki zao na wamekuwa
wakiwapa hata wachezaji kwa mkopo. Hivyo hakuna ubaya kuwasaidia kipindi
hiki wana shida, tena inayohusisha taifa.
0 comments:
Post a Comment