Upande wa Jamhuri umeiomba Mahakama Kuu ya Tanzania kuhimiza uwepo wa Katibu ya Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda mahakamani hapo Juni 30, mwaka huu wakati usikilizwaji wa rufaa dhidi yake utakapoanza.
Wakili Mkuu Mwandamizi wa Serikali, Bernard Kongola akitoa ombi hilo mbele ya Jaji, Edson Mkasimongwa, wakati wa usikilizwaji wa rufaa ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) dhidi ya Sheikh Ponda akipinga kuachiliwa huru kwa kiongozi huyo.
Awali wakili wa utetezi, Abubakar Salum aliiomba mahakama kusogeza mbele tarehe ya rufaa hiyo kwakuwa ndio kwanza alikuwa amepata jadala la rufaa hiyo na hivyo asingeweza kujenga hoja zake papo kwa hapo.
Rufaa hiyo itasikilizwa Juni 30, mwaka huu.
Mwishoni mwa mwezi Novemba, mwaka jana, Mahakama ya Hakimu Mkazi
Morogoro ilimuachia huru Sheikh Issa Ponda aliyekuwa akituhumiwa kwa
makosa ya uchochezi baada ya mahakama hiyo kutoridhishwa na ushahidi wa
upande wa mashtaka na hivyo kumuona hana hata
Awali kabisa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Morogoro,
Richard Kabate, Mwanasheria Kiongozi wa Serikali, Bernard Kongola,
alidai kuwa Agosti 10, mwaka 2013, katika eneo la Uwanja wa Ndege,
Manispaa ya Morogoro, Ponda aliwaambia Waislamu wasikubali uundwaji wa
kamati za ulinzi na usalama za misikiti, kwa madai kuwa zimeundwa na
BAKWATA, ambao ni vibaraka wa CCM na serikali.
Alidai kuwa Sheikh Ponda ambaye alikuwa anatetewa na wakili wa
kujitegemea Juma Nassor aliwaagiza waumini hao kuwa endapo watu hao
watajitokeza kwao na kujitabulisha kwamba ni kamati za ulinzi na usalama
za misikiti, wafunge milango na madirisha wawapige.Ilielezwa kuwa kauli hiyo ni kinyume cha agizo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, iliyotolewa na Hakimu Victoria Nongwa Mei 9, mwaka 2010, ambayo ilimtaka Ponda ndani ya mwaka mzima kuhubiri amani na Kuwa Raia Mwema.
Katika shitaka la pili, Kongola alidai kuwa Agosti 10, mwaka huu, katika eneo la Uwanja wa Ndege, Morogoro, Ponda aliwaambia Waislamu kuwa serikali ilipeleka jeshi Mtwara kushughulikia suala la vurugu iliyotokana na gesi ili kuwaua, kuwabaka na kuwatesa wananchi, kwa sababu asilimia 90 ya wakazi hao ni Waislamu.
Kwamba, Ponda aliwaambia wafuasi wake kuwa serikali haikufanya hivyo kwa wananchi wa Loliondo walipokataa Mwarabu asipatiwe kipande cha ardhi ya uwindaji baada ya kudai ni mali yao, kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wa huko ni Wakristu.
Shitaka la tatu ambalo linafafana na lile la pili, ambalo nalo linadaiwa kutendwa Agosti 10, mwaka huu, ambapo kauli ya Ponda inadaiwa kuumiza imani za watu wengine kinyume cha kifungu cha sheria namba 390 na kanuni ya adhabu namba 35 cha mwaka 2002.
0 comments:
Post a Comment