NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Sakata la wanafunzi 7802: Wabunge CCM, Upinzani ‘wakinukisha’ bungeni

[UNSET]

Hali ya vurugu imetokea bungeni baada ya Naibu Spika, Tulia Ackson kutupilia mbali ombi la Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari kutaka muongozo wa Spika juu ya wanafunzi 7,802 wa Chuo Kikuu cha Dodoma kusimamishwa masomo  chuoni hapo jana.

Vurugu hizo zilizosababisha kuahirishwa kwa shughuli za bunge hadi saa 10, zilizofanywa na wabunge wa chama kilichopo madarakani, CCM na vyama vya upinzani, vililenga katika kumshinikiza Naibu Spika kutoa nafasi kwa wabunge kujadili suala hilo kama ‘hoja ya dharura’.

Takribani wanafunzi 7,802 wa kozi maalumu ya ualimu wa sayansi kwa ngazi ya stashahada walitakiwa waondoke chuoni hapo mara moja ili kuipisha serikali kupitia wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi kuipitia upya kozi yao kutokana na matatizo yaliyopo katika ufundishaji wa stashahada hiyo

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya bunge, Mbunge Nasari amesema alichokifanya naibu spika si sawa kwani wabunge wote walikua na nia ya kuwatetea wanafunzi hao ambao kwa sasa wanaishi kwa shida mjini Dodoma na hata bunge litakaporejea saa kumi, bado watataka suala hilo lijadiliwe.

“Hoja iko pale pale tatizo hili ni la dharura vinginevyo na hili bunge lifungwe tuondoke kwa sababu kuna watu zaidi ya 7,000 ambao wapo mtaani hatujui hatima yao ni nini,” alisema Nassari.
Mapema asubuhi ya leo, wabunge wanaounda kambi rasmi ya upinzani bungeni walitoka nje ya bunge ili kupisha kuapishwa kwa wajumbe watano wa baraza la wawakilishi kutoka Zanzibar.

Walisema sababu ya kutoka nje ni kutoutambua uchaguzi wa marejeo uliofanyika Machi 20, mwaka huu.
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment