Mifuko ya plastiki inayofungasha pombe maarufu kama ‘viroba’ imepigwa marufuku na Serikali kuanzia mwakani.
Sambamba na hilo Serikali pia, imepiga marufuku moja kwa moja utengenezaji, usambazaji, uingizaji nchini wa mifuko ya plastiki kuanzia mwaka huo.
Waziri
wa Nchi , Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January
Makamba aliwaambia wanahabari jana sehemu kubwa ya mifuko hiyo
inayotolewa bure imekuwa ikichangia uchafuzi wa mazingira kwa kiasi
kikubwa.
Wakati
Makamba akiyasema hayo, Februari mwaka huu Naibu Waziri Ofisi ya Makamu
wa Rais (Muungano na Mazingira), Luhaga Mpina aliondoa zuio la matumizi
ya mifuko ya plastiki akisema kuwa itaziweka rehani ajira za Watanzania
wanaofanya kazi kwenye viwanda vinavyotengeneza mifuko hiyo.
Pia, Mpina alisema itapunguza kasi ya uwekezaji wa viwanda vilivyowekeza katika bidhaa hiyo.
Akizungumza
katika siku ya Mazingira Afrika, Mkurugenzi wa Mazingira, Dk Julius
Ningu alisema maamuzi hayo yamelenga kulinda viwanda vilivyoajiri mamia
ya Watanzania, tofauti na nchi nyingine zinazotegemea wazalishaji wa nje
ya nchi.
Makamba
akizungumzia uamuzi mpya wa kuzuia mifuko ya plastiki, alisema matumizi
ya mifuko inayofungashia vileo na inayotumika katika matumizi mengine
husambaa na kuchafua mazingira. Alisema mifuko ya plastiki inatajwa
kuziba mifereji na kusababisha mafuriko na athari nyingine za mazingira.
“Leo
(Jana), tumeamua kutangaza ili kuwaanda wahusika wasiendelee kuwekeza
katika mifuko hii badala yake wasubiri utaratibu mwingine utakaowekwa na
Serikali,” alisema Makamba na kuongeza kuwa:
“Asilimia kubwa ya uchafu kwenye nyanzo vya maji, mito, maziwa na fukwe za bahari ni mifuko ya plastiki.”
Makamba ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli, alisema Serikali inakamilisha majadiliano ya ndani na baadaye itawahusisha wadau kuhusu dhamira ya kupiga marufuku ya moja kwa moja mifuko hiyo.
Makamba ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli, alisema Serikali inakamilisha majadiliano ya ndani na baadaye itawahusisha wadau kuhusu dhamira ya kupiga marufuku ya moja kwa moja mifuko hiyo.
Alifafanua
kwamba Serikali itatoa muda kwa walioajiriwa, kujiajiri na kuwekeza
kwenye biashara ya mifuko hiyo ili kujiandaa kuacha shughuli hizo na
badala yake itawezesha mazingira ya utengenezaji na upatikanaji wa
vifungashio mbadala.
“Kwa
wanaotengeza mifuko hii na kuiuza katika soko la nje hatuna tatizo nao
waendelee. Ila kwa soko la ndani hawataruhusiwa kufanya hivyo.Zuio hili
litakuwa la kisheria siyo kwa maneno,” alisisitiza Makamba.
Aliongeza kuwa katika kuonyesha Serikali imedhamiria kupambana na hali hiyo wizara yake imeamua kutuma timu ya watu watano kwenda Rwanda kujifunza namna bora ya kudhibiti matumizi na kuzuia mifuko hiyo tangu mwaka 2008.
Aliongeza kuwa katika kuonyesha Serikali imedhamiria kupambana na hali hiyo wizara yake imeamua kutuma timu ya watu watano kwenda Rwanda kujifunza namna bora ya kudhibiti matumizi na kuzuia mifuko hiyo tangu mwaka 2008.
Waziri
huyo alitoa wito kwa watengenezaji, wasambazaji na waagizaji wa mifuko
hiyo kujiandaa na zuio hilo na katika siku zijazo Serikali itatoa
utaratibu na maelekezo ya tarehe ya kuanza zuio huku taratibu nyingine
za kina zikifuata ili kuondoa mkanganyiko.
Katika
hatua nyingine, Makamba alisema maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya
Mazingira Duniani ambayo hufanyika Juni 5 kila mwaka hayatafanyika
kitaifa badala yake wizara imewaelekeza wakuu wa mikoa kufanya
maadhimisho katika maeneo yao.
“Tumewapa
miongozo kuhusu utekezezaji wa shughuli hizo za maadhimisho zinazolenga
kutoa hamasa ya hifadhi ya mazingira hususan nyanzo ya maji amabayo ni
muhimu kwa viumbe hai,” alisema Makamba.
Kwa
mujibu wa Makamba, kauli mbiu ya mwaka huu kitaifa juu ya maadhimisho
hayo ni ‘ tuhifadhi vyanzo vya maji kwa uhai wa taifa letu’aliwashauri
na kuwataka Watanzania kutumia siku hiyo kupanda miti, kudhibiti
uchomaji wa misitu
Ofisa Mwandamizi Mazingira wa Nemc, Arnold Kisagala alisema nusu ya mifuko ya plastiki nchini inazalishwa na kuingizwa kutoka nchi jirani ya Kenya.
Ofisa Mwandamizi Mazingira wa Nemc, Arnold Kisagala alisema nusu ya mifuko ya plastiki nchini inazalishwa na kuingizwa kutoka nchi jirani ya Kenya.
Alisema
agizo la Waziri Makamba litawezekana, lakini linahitaji ushirikiano
kutoka kwenye sekta zingine kwa kuwa viwanda vingi vya mifuko ya
plastiki vipo Kenya.
chanzo>mpekuzi
0 comments:
Post a Comment