NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Maalim: Dkt. Shein ataondoka kwa presha ya wananchi



01-maalim-Seif

Katibu mkuu wa chama cha wananchi (CUF), Maalim Seif Hamad amesema Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein , ataondoka madarakani kwa presha ya wananchi ya kutomtambua yeye na viongozi wa serikali yake kama viongozi halali.

Maalim Seif alitoa tamko hilo alipokuwa akizungumza na viongozi watendaji kwenye ofisi za CUF Bumbwini, Unguja na kuongeza kuwa vikwazo vya wahisani vinavyoendelea kuchukuliwa kutokana na kufutwa na matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 25 ni ishara nyingine inayoonesha Rais Shein na serikali yake hawataweza kuiongoza Zanzibar kwa muda mrefu.

“Tutaendelea kudai haki yetu kwa njia ya amani ndani na nje ya nchi mpaka Dk. Shein aondoke madarakani kwa presha ya wananchi bila ya kusukumwa au kupigwa kofi,” alisema.
Aidha, alisema wakati umefika kwa jeshi la polisi kuacha kutumiwa vibaya na viongozi kuwanyanyasa viongozi na wanachama wa CUF kwani hali hiyo itasababisha chuki za kisiasa kurudi Zanzibar.
Awali, msafara wa Maalim Seif ulikwama baada ya kufika kona ya Bumbwini Michungwa Miwili na kukuta polisi wakiongozwa na Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kaskazini Unguja, Aziza Toufiq, wamefunga njia kwa kuweka kizuizi huku askari wa FFU wakiwa na mabomu ya machozi, wakitoa sababu za kutoruhusu kufanyika kwa mkutano huo.
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment