NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

SYMBION WAIBURUZA TANESCO MAHAKAMANI


Licha ya Rais John Magufuli kuisisitiza TANESCO kuepukana na mikataba ya “ajabu ajabu” na kulitia Taifa na shirika hasara, bado TANESCO mwezi Desemba walisaini mkataba wa miaka 15 na Kampuni ya Symbion, na baada ya “agizo” hilo la Rais wakati akifungua mitambo ya umeme wa Gas wa Kinyerezi

Hali hiyo imeifanya Tanesco kuamua “kusitisha” aina yoyote ya mahusiano ya kimkataba na Kampuni ya Symbion,hivyo kuifanya Symbion kuchukua hatua zaidi za kuishtaki Tanesco Mahakamani.

Kila mwezi Tanesco hulipa ktakribani shilingi bilioni 36 kwa makampuni ambayo imeingia nayo mikataba ya kuzalisha umeme, malipo hayo ni kwa ajili ya Capacity Charge kitu ambacho huliingiza Taifa na shirika lenyewe hasara kubwa na kuongeza mzigo wa malipo kwa wananchi wa chini.

Wakati Tanesco ikichukua maamuzi hayo chini ya “influence” ya Rais,wao Symbion wanasema hawautambui msimamo huo mpya wa Tanesco kwani Desemba mwaka wa jana 2015,Symbion na Tanesco walishaingia kwenye mkataba wa miaka 15 wa Symbion kuliuzia Shirika la Umeme Tanzania kiwango cha umeme.

Management ya Symbion imechukuwa hatua ya kuifikisha Tanesco mahakamani ili kuishinikiza iweze kuendelea na mkataba huo ambao Symbion ingemuuzia Tanesco umeme kwa miaka 15.

CHANZO: THE CITIZEN
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment