Zaidi
ya tani 154 za sukari inayodaiwa kufichwa kwenye maghala na
mfanyabiashara mkubwa wa bidhaa hiyo mkoani Dodoma zimezuiliwa na
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Maofisa wa Jeshi
la Polisi ili kupisha uchunguzi na endapo itabainika kuwa ilifichwa
makusudi muhusika atachukulia hatua kulingana na maagizo yaliyotolewa na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli.
Shehena hiyo imebainika kufuatia msako
uliofanywa usiku na TAKUKURU na Jeshi la Polisi baada ya kupata taarifa
ya uwepo wa sukari kwenye maghala hayo ambapo Mkuu wa TAKUKURU mkoani
Dodoma Emma Kuhanga amesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na endapo
itabainika kuna hujuma ndani yake hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi
ya muhusika.
Kwa upande wake mmoja kati ya watunza
ghala aliyefahamika kwa jina moja la Samir aliyekutwa eneo la tukio
wakati wa msako amekanusha kufichwa kwa sukari hiyo huku akidai kuwa
inauzwa sokoni kila siku kwa utaratibu maalum.
Wakati sakata la uhaba wa sukari
likiendelea kutikisa nchi nzima Jukwaa Huru la Wazalendo Tanzania
limetoa tamko la kulaani wafanyabiashara wanaohujumu upatikanaji wa
bidhaa hiyo huku makundi mbalimbali ya jamii yakiendelea kupaza sauti
kuitaka serikali itafute suluhisho mapema kwani wanaoumia asilimia kubwa
ni wananchi wa maisha ya kawaida.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
TAKUKURU yazuia Tan 154 za sukari Dodoma
Reviewed by Newspointtz
on
15:33:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment