Kuna majina ukiyasikia katika tasnia ya
muziki hapa Tanzania unaweza ukawa unafurahi mwenyewe bila hata ya
kuambiwa ufurahi, uzuri wake hicho anacho kiimba ndicho anakifanyia kazi
kwa sasa. unaweza kufikiri ninani huyo? jibu Joseph Haule a.k.a Profesa
Jay ambaye hivi sasa ni Mbunge wa Jimbo la Mikumi.
PROFESA JAY NI NANI?
Profesa Jay amefanya makubwa katika
muziki wa Tanzania pengine nyimbo zake alizokuwa anatunga ndizo
zilizomfanya ajiamini na kujitosa katika siasa, hivi unakumbuka kibao
kilichoitwa Ndiyo Mzee?Kikao cha Dharura?Nang’atuka? zote hizo zilihusu siasa na watu walikuwa wanadhani siku moja atakuwa kingozi wa siasa na hatimae imekuwa kweli.
ATABIRI HAYA KWA WASANII WA HIPHOP
Prof. Jay amefunguka na kuwamwagia sifa
wasanii wanaofanya muziki wa HipHop kwa kazi nzuri walizo zifanya
akiamini huenda wasanii hao wakawa na vitu vya ziada huku akitolea
mifano ya mashairi kama ya wasanii Kala Jeremiah, Roma, Nick wa pili na
Mwana Fa .
“Wasanii
wanamsimamo na wana shule kazi ya ubunge inatakiwa ujipange kwa ajili
ya kuwatumikia wananchi, wasani hao wanavitu kulingana na mashairi yao
labda tu bado wanahofia kushika peni na karatasi ushakuwa kiongozi”Maneno ya Profesa Jay.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
UTABIRI WA PROFESA JAY KWA WASANII WA HIPHOP
Reviewed by Newspointtz
on
15:36:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment