WABUNGE
wanawake 53 wa kambi ya upinzani kutoka vyama vya CUF na Chadema
wamejitoa kwenye Umoja wa Wabunge Wanawake (TWPG) baada ya kutoombwa
radhi na Mbunge la Ulanga, Godluck Mlinga (CCM) aliyesema wabunge hao
kutoka Chadema walipata ubunge kwa njia ya mapenzi.
Mlinga
alisema wabunge wanawake ndani ya Chadema, walipata nafasi hiyo baada
ya kuwa ‘baby’ wa watu. Alitoa kauli hiyo wakati anachangia Makadirio ya
Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha
2016/2017 bungeni Mei 5 mwaka huu.
Sambamba
na hilo, alisema wabunge wa ndani ya chama hicho wamo pia wenye
uhusiano wa jinsia moja. Hata hivyo hakuwataja kwa majina wabunge hao.
“Kila
mwanamke ndani ya chadema kaingia ubunge kwa sifa yake lakini sifa
kubwa ni lazima uwe baby (mpenzi) wa mtu. Ndani ya Chadema kuna wapenzi
wa jinsia moja,” alisema Mlinga.
Katika
barua yao ya kujitoa jana iliyosainiwa na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee
kwa niaba ya wabunge wenzake wa kambi ya upinzani na nakala kupewa
Spika, Job Ndugai, ilieleza kuwa kauli ya Mlinga inadhalilisha wabunge
hao, utu na heshima ya mwanamke.
“Licha
ya juhudi zilizofanywa na wabunge wa upinzani za kutaka mbunge
husika(Mlinga) afute kauli yake , juhudi hizo hazikuzaa matunda kutokana
na Naibu Spika(Tulia Ackson) kupuuza miongozo iliyokuwa ikiombwa.
"Na
kikubwa alichokifanya baada ya mbunge (Mlinga) kumaliza kutukana ni
kuwataka watu wa hansard wafute kwenye kumbukumbu za Bunge, kitu ambacho
ni kinyume na matakwa ya Kanuni za Bunge,”alisema Mdee kwenye barua hiyo iliyosainiwa na wabunge wa CUF 10 na wa Chadema 43.
Alisema
wabunge wa upinzani walisononeshwa zaidi na wabunge wenzao wanawake wa
CCM, wakiongozwa na aliyekuwa Katibu wa TWPG, Angela Kairuki na Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge,Vijana, Ulemavu na
Ajira, Jenista Mhagama kushangilia udhalilishaji huo.
“Ukimya
wenu kwenye matukio haya na ushiriki wenu katika kushangilia wakati
wanawake wanadhalilishwa inatufanya tuhoji mantiki ya uwepo wetu katika
umoja huu ambao tunaambiwa malengo na dhamira yake ni kutuunganisha
wanawake katika kumkomboa, kumpigania na kulinda haki na utu wa
mwanamke,” alisema Mdee.
Wabunge
hawa wanajitoa licha ya baada ya tukio hilo, umoja huo kupitia kwa
Mwenyekiti wake, Margaret Sitta kulaani na kueleza kutokubaliana na
tabia ya baadhi ya wabunge ya kutumia lugha za matusi, kejeli ,dharau na
udhalilishaji wa wabunge wanawake kutoka Chadema kuwa wamepata nafasi
hiyo kwa njia ya kuwa ‘baby’ wa mtu.
0 comments:
Post a Comment