NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Wema Sepetu azindua Application yake mbele ya Waziri Nape Nnauye.

Mwigizaji wa filamu Tanzania Wema Sepetu ametangaza rasmi Application yake 22 May 2016 ikiwa ni njia rahisi zaidi ya kujiweka karibu na mashabiki wake.

Kupitia mfumo wa APP na SMS utaweza kupata habari,picha na video clips za maisha ya Wema Sepetu. Uzinduzi wa APP hii ulihuthuriwa na Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo Mh Nape Nnauye.

Application hii itahusisha wale watumiaji wa simu za Smartphone na hata ambao si watumiaji wa Smartphone pia,Kama unatumia Smartphone unaweza kudownload Application hiyo kama zingine tu ila wasio na Simu za Smartphone watajiunga kwa kutuma neno wema kwenda 15404 na watakuwa wanapokea meseji mbili kila siku za matukio yanayomuhusu Wema Sepetu.

Haya ni maelezo ya Wema Sepetu kutoa IG Yake.
Kwanza Kabisa nichukue nafasi hii Kusema Asante Mungu wangu kwa kunifanikisha kukamilisha kile ambacho nimekuwa nikikitamani na ambacho nimefanyia kazi kwa takribani ya miezi Mitano mpaka kufika siku hii ya leo… Lakini pia niseme Asante kwa Familia yangu yote kwa ujumla, Bila kusahau mashabiki wangu wapenzi kwa kunipa moyo wa kutokukata tamaa japokuwa kuna mengi ambayo kwa binadamu wa kawaida huwezi vumilia Ila kiukweli mashabiki wangu mmekuwa mnanipa nguvu na Courage everyday… Najisikia Fahari sana Leo hii kuwa Mwanamke wa Kwanza Barani Africa Kuwa na MobileApp inayonitangaza mimi Mwenyewe kama Content…. Kwa kutumia hii App unaweza kupata chance ya kupata zile habari zote za uhakika kuhusu Wema Sepetu… Kuna vingi ambavyo pia unaweza kupata kama Video Clips, Audio na Pictures kwa wale watumiaji wa Smart Phone… Lakini pia kwa wale wasio na Smart phone basi unapata Habari na Matukio mbali mbali kuhusu mimi ambayo sio Longo longo… Trust me with this app kuna mengi saaana mtakayoyapata… Ni Rahisi sana Una tuma Neno “Wema” kwenda namba 15404 and u are done…. Asanteni sana…. Nawapenda Mno… Huduma hii ipo Applicable kwa Mitandao Yote Tanzania…. What are u waiting for…?

Hongera Wema Sepetu.


Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment