
Russia itakutana na rungu la Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) baada ya mashabiki wake kuwashambulia na kuwaumiza wale wa England.
Vurugu
kubwa zilitokea wakati wa mechi ya kwanza ya michuano ya Euro 2016
jijini Marseille nchini Ufaransa wakati England na Russia zilipomaliza
dakika 90 kwa sare ya bao 1-1.
Mashabiki hao walirusha moto na kupiga bunduki za mwangwi zinazotoa moto wa miale, jambo ambalo Uefa inaona si sahihi.
Mashabiki
wa England pamoja na kuonekana au kujulikana ni wajeuri, lakini
walilazimika kukimbia kutokana na vurugu hizo ambazo awali zilianza hata
kabla ya mechi.
0 comments:
Post a Comment