NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

UONGOZI MPYA WA YANGA UMETANGAZWA BAADA YA KURA ZOTE KUHESABIWA


Wajumbe wa kamati ya uchaguzi ya Yanga, wakihesabu kura za wagombea
Wajumbe wa kamati ya uchaguzi ya Yanga, wakihesabu kura za wagombea
Yusuf Manji ameshinda nafasi ya uenyekiti wa Yanga kiulaini kutokana na kutokuwa na mpinzani kwenye nafasi hiyo hivyo kupita bila kupingwa kwenye nafasi ambayo alikuwa akiitetea.
Clemen Sanga nae amepenya katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti kwa kumbwaga mpinzani wake Titus Osoro.
Shughuli pevu ilikuwa kwa wagombea nafasi ya ujumbe ambapo jumla ya wagombea 20 walikuwa wakiwania nafasi 8 za ujumbe.

Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya Yanga Sam Mapande (katikati) akitangaza matokeo ya uchaguzi mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kuhesabu kura
Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya Yanga Sam Mapande (katikati) akitangaza matokeo ya uchaguzi mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kuhesabu kura
Mwenyekiti
Yusuf Manji ameibuka mshindi wa nafasi ya uenyekiti akipenya bila kupingwa na kupata idadi ya kura 1468 kati ya 1,470 zilizopigwa na wanachama, huku kura 2 pekee zikiwa zimeharibika.
Makamu Mwenyekiti
Clement Sanga amemgaragaza mpinzani wake baada ya kupata kura 1428 kati ya 1,508 zilizopigwa wakati mpinzani wake Titus Osoro akiambulia kura 80 pekee.
Wajumbe
Ayoub Nyenzi (889), Salim Mkemi (894), Bakar Malima (577), Godfrey Mheluka (430), David Ruhago (582), Lameck Nyambaya (655), Sylvester Haule (197), Pascal Laizer (178), Samwel Lukumay (818), Hashim Abdallah (727), George Manyama (249), Hussein Nyika (770), Siza Lyimo (1027), Beda Tindwa (452),Tobias Lingalangala (889), Athumani Kihamia (558), Mchafu Chakoma (69), Edgar W  Chibura (72), Ramadhani M. Kampira (182), Omary S. Amei (1069)
Kwa Matokeo hayo, uongozi mpya wa Yanga uliochaguliwa na wanachama unaundwa na Mwenyekiti Yusuf Manji, Makamu Mwenyekiti Clement Sanga huku wajumbe wakiwa ni Omary S. Amei, Siza Lyimo, Salim Mkemi, Tobias Lingalangala, Ayoub Nyenzi, Samwel Lukumay, Hussein Nyika na Hashim Abdallah.

Baadhi ya wagombea nafasi ya ujumbe walioshinda uchaguzi katika picha ya pamoja
Baadhi ya wagombea nafasi ya ujumbe walioshinda uchaguzi katika picha ya pamoja
Kura zahesabiwa usiku kucha

Wanachama na mashabiki wa Yanga iliwabidi kukesha kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee wakisubiri matokeo ya uchaguzi
Wanachama na mashabiki wa Yanga iliwabidi kukesha kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee wakisubiri matokeo ya uchaguzi
Zoezi la uchaguzi wa Yanga lilianza jana asubuhi na kudumu kwa siku nzima, mchakato wa kuhesabu kura za wagombea ulianza jana jioni ambapo kura za Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti zilihesabiwa na kumalizika mapema lakini ‘mziki’ ulikuwa kwenye kura za wajumbe ambapo ilibidi kamati ya uchaguzi ikeshe ikihesabu kura na hatimaye kutangaza matokeo leo asubuhi.
Mwanamama awaburuza vidume

Mwanamama Siza Lyimo (kulia) akipongezwa na watu wake wa karibu baada ya kuchaguliwa kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga kwa kupata kura 1027 akishika nafasi ya pili nyuma ya Omary S. Amei aliyepata kura 1069
Mwanamama Siza Lyimo (kulia) akipongezwa na watu wake wa karibu baada ya kuchaguliwa kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga kwa kupata kura 1027 akishika nafasi ya pili nyuma ya Omary S. Amei aliyepata kura 1069
Siza Lyimo alikuwa ni mwanamke pekee aliyegombea nafasi ya uongozi kwenye klabu ya Yanga, akizungukwa na wanaume 19 kwenye kinyang’anyiro cha nafasi ya ujumbe wa kamati tendaji alifanikiwa kushika nafasi ya pili baada ya kupata jumla ya kura za ndiyo 1027 huku Omary S. Amei aliyepata kura 1069 akiwa ni mwanaume pekee aliyemshinda mwanamama huyo kwenye nafasi ya ujumbe.
Dondoo kwa namba:
23 ni idadi ya wagombea wote waliokuwa wakigombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye klabu ya Yanga kuanzia nafasi ya Mwenyeti, Makamu Mwenyekiti na Ujumbe.
20-hii ni idadadi ya wagombea wa nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga
8-ni idadi ya nafasi za ujumbe ambazo zilikuwa zikiwaniwa na wagombea waliokuwa 20
2-ni idadi ya wagombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti
1-nafasi ya Uenyekiti ilikuwa ikigombewa na mtu mmoja tu ambaye aligombea bila kupingwa, ni namba pia ambayo inamwakilisha mwanamama Siza Lyimo ambaye alikuwa mgombea pekee wa kike aliyejitokeza kugombea ujumbe katika uchaguzi huo.
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment